26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Vifo majeruhi ajali ya moto vyaendelea kuongezeka

AVELINE KITOMARY – DAR ES SALAAM

IDADI ya vifo vya ajali ya lori la mafuta iliyotokea mkoani Morogoro Agosti 10, vimeendelea kuongezeka baada ya majeruhi mwingine kufariki usiku wa kuamkia jana na kufanya idadi sasa kufikia 94.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Aminieli Aligaesha, alisema idadi ya majeruhi waliobaki hospitali hapo ni 20 huku 26 kati ya 46 waliofikishwa hapo Agosti 11 wakiwa wameshafariki dunia.

 Aligaesha alisema majeruhi waliobaki wanaendelea kupatiwa matibabu katika vyumba vya uangalizi maalumu (ICU) kwenye jengo la Mwaisela.

“Usiku wa kuamkia leo (jana) tumepoteza majeruhi mmoja na sasa wamebaki 20 kati ya 46 walioletwa hapa Muhimbili, wengine 26 wameshapoteza maisha na waliobaki wote wako ICU jengo la Mwaisela wanaendelea kupatiwa matibabu,”alisema Aligaesha.

Alisema  madaktari  wanaendelea kuwapatia matibabu ya hali ya juu majeruhi waliobaki bila kujali wamepata madhara kiasi gani.

 “Sisi hatujali majeruhi wameungua kwa kiasi gani, wote lazima tuwahudumie  ili kuokoa maisha yao, hatujakata tama mpaka sasa, majeruhi wako katika uangalizi na kila majeruhi ana muuguzi wake,”alisema Aligaeshi.

Kati ya Majeruhi 46 waliofikishwa Muhimbili Jumapili ya juma lililopiya, siku hiyo usiku walipoteza maisha watatu, Jumatatu wanne, Jumanne mmoja, Juma tano sita, Alhamisi saba, Ijumaa wanne na usiku wa kuamkia jana mmoja.

Watu wazidi kujitolea damu

Wakati huohuo, hospitali hiyo imepokea chupa 100 za damu kutoka kwa Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agrey Mwanri, kwaajili ya majeruhi hao.

Akipokea msaada huo Aligaesha alisema tangu kutokea kwa ajali hiyp, hospitali hiyo imepata chupa 611 za damu kutokana na makundi mbalimbali.

 “Tunawashukuru wadau na vikundi mbalimbali ambavyo vinajitokeza kusaidia kuchangia damu kwaaji ya majeruhi na wagonjwa hawa, niwashukuru viongozi wa Serikali na binafsi hasa wakuu wa mikoa katika kuhamasisha utoaji damu.

 “Leo (jana) tumepokea unit 100 kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora kupitia wenzetu wa damu salama wa Mkoa huo na pia tunatambua jitihada ya mikoa mingine na tumekusanya damu nyingi tangu Jumamosi na hizi za leo zimefikia unit 611 hii inaonesha ni jinsi gani Watanzania wanakuwa wamoja majanga yanapotokea,” alisema Aligaesha.    

Kwa upande wake Mwakilishi huyo wa ambaye pia ni Meneja Mpango wa Damu Salama, Dk. Magdelena Lyimo, alisema wataendendelea kuhamasisha watu kuchangia damu kwa wagonjwa wengi hata baada ya ajali ya moto.

“Damu bado inahitajika hata kwa wagonjwa wengine, tutaendelea kuhamasisaha utoaji damu  kwa makundi na wadau mbalimbali ili kupata damu nyingi zaidi,”alisema Dk. Lyimo.

MISAADA YAENDELEA

Pia wadau mbalimbali wameendelea kutoa misaada ya vifaa kwaajili ya majeruhi hao.

Jana Katibu wa Umoja wa Distuct UIIC Lions Clubs, Shabbir Khalfan, alisema wametoa msaada wa zaidi ya Sh milioni 2.5 ili kuwafariji wahanga  hao.

“ Tuko hapa kuwapa tulicho nacho majeruhi wa ajali ya moto vifaa hivi vimegharimu kiasi cha Sh milioni 2.5, tumenunua pamba, maji, madawa mbalimbali kwaajili ya majeruhi hawa nawaambia tuko pamoja katika kipindi hiki  cha shida,”alisema Khalifan.

Akipokea msaada huo Mkuu wa idara ya Utasishaji MNH Dk. Batusaje John, aliishukuru taasisi hiyo na kusema vifaa hivyo vinamsaada mkubwa kwa majeruhi hao.

Alisema bado wanauhitaji wa vifaa kama Vaselini na pamba kwaajili ya wagonjwa hao kwani yanamatumizi makubwa kwao.

“ Tunashukuru kwa msaada tuliopata kutoka kwa hiki kikundi, vitu hivi vitawasaidia wagonjwa na pia tunaupungufu wa gozi, Vaseline na pamba tunaomba wadau watoe msaada wa vitu hivyo,”alisema Batusaje.

Mwishoooooo

DSE watakiwa kujiimarisha

Na Mwandishi wetu

-Dar es Salaam

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Khatibu Kazungu, amelitaka Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), kuendelea kujiimarisha kwa kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kuwekeza zaidi katika soko hilo.

Dk Kazungu alisema hayo alipofanya ziara katika soko hilo ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 katika taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.

Alisema watu takribani 500,000 ambao wamewekeza katika soko hilo ni ndogo ikilinganisha na Watanzania wote ambao ni zaidi ya milioni 50.

Alisema ni vema DSE ikatumia majukwaa mbalimbali kuhamasisha wananchi kushiriki katika soko hilo ili kukuza kipato chao kutokana na faida zake.

Alisema ushiriki wa watu wengi katika soko hilo hususani walio katika sekta ya uvuvi, mifugo na kilimo, kutaongeza chachu ya maendeleo yao na Taifa.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa DSE, Moremi Marwa, alisema DSE ipo kwa ajili ya kuwezesha wawekezaji kuwekeza katika maeneneo mbalimbali kulingana na bidhaa zilizopo sokoni.

Alisema ili kupata bidhaa zaidi, DSE imekuwa ikifanya juhudi kwa kushirikiana na wadau wengine ili kuziwezesha Serikali za Mitaa na halmashauri za miji na majiji kuweza kupata fedha kupitia mifumo ya masoko ya mitaji.

Alieleza kuwa mifumo ya masoko ya mitaji katika halmashauri italeta wigo mwingine wa upatikaji wa fedha kwa ajili ya kujenga miradi ya miundombinu na viwanda katika miji na majiji nchini.

 “Soko la DSE limekua kutoka Sh trilioni 16 hadi trilioni 20 katika kipindi cha miaka minne,  hati fungani Sh trilioni 3.5 hadi trilioni 9.5 na kwa wawekezaji kutoka  220,000 na sasa 550,000

“Ukwasi na miamala sokoni imeongezeka kutoka wastani wa  Sh bilioni 50 kwa mwaka hadi zaidi Sh bilioni 500  kwa mwaka na katika miamala na ukwasi wa hati fungani kutoka wastani wa Sh bilioni 300 hadi kufikia wastani wa Sh bilioni 900 kwa mwaka” alisema Marwa.

Alisema kuwa DSE ina bidhaa kuu tatu zilizopo sokoni ambazo mwananchi yeyote anaweza kuwekeza, bidhaa hizo ni hisa, ambapo kuna kampuni 28 zilizoorodheshwa sokoni zenye thamani ya Sh bilioni 19.2.

Bidhaa nyingine ni hati fungani za Serikali zenye thamani ya Sh bilioni 9.5 na pia Hati fungani za makampuni binafsi zenye thamani ya Sh bilioni 250.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles