23.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 20, 2021

UN yaonya uwezekano wa uhalifu wa kivita DRC

 NEW YORK, MAREKANI

UMOJA wa Mataifa (UN) umetahadahrisha kuwa kuna uwezekano wa kujiri uhalifu wa kivita Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), baada ya watu kadhaa kuuawa na makundi ya watu wenye silaha.

Ofisi ya Pamoja ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (UNJHRO) imechapisha ripoti inayosema mauaji, vitendo vya kikatili, ubakaji na vitendo vingine vinavyokiuka sheria za haki za binadamu vimekithiria na vinatekelezwa na wanamgambo wenye silaha Kaskazini Mashariki mwa DRC, hasa kabila la Walendu.

Ripoti hiyo ilisema vitendo hivyo vinaweza kuwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Katika ripoti yake, Ofisi ya UNJHRO ilisema katika kipindi cha miezi sita iliyopita, watu wasiopungua 296 wameuawa, 151 kueruhiwa na wengine 38 kubakwa, wakiwamo wanawake na watoto.

UNJHRO ilisema vitendo hivyo vya kikatili vilitekelezwa na waasi kutoka kabila la Walendu kati ya mwezi Novemba mwaka uliopita na mwezi Aprili mwaka huu.

Baada ya miaka kadhaa ya utulivu, ghasia za kikabila zimeongezeka tangu mwezi Desemba 2017, hasa kutokana na mizozo ya ardhi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,961FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles