26.8 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Umakini waitesa Stars

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAMA

TIMU ya Taifa Tanzania, ‘Taifa Stars’  jana ilianza kwa kusuasua kampeni zake za kusaka tiketi ya kushiriki fainali za  mataifa ya Afrika, kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani(Chan), baada ya kulazimishwa suluhu na Kenya, katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Huo ulikuwa mchezo wa pili kwa timu hizo kukutana katika mashindano mawili tofauti  yanayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf), katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja.

Awali zilikutana katika hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon), iliyofanyika nchini Misri, ambapo Taifa Stars ilichapwa mabao 3-2.

Mchezo wa marudiano kati ya  timu hizo utapigwa Agosti 4 jijini Nairobi, Kenya, ambapo mshindi atakutana na Sudan kabla ya mbabe kutinga hatua ya makundi.

Mchezo wa jana ulioanza kwa kasi kwa pande zote, dakika ya pili John Bocco alikosa bao baada ya kupokea pasi ya Hassan Dilunga lakini mkwaju wake ulitoka nje.

Dakika moja baadaye, mpira wa kichwa uliopigwa na Idd Selemani ‘Nado’, akiunganisha krosi ya Paul Godfrey  ulitoka nje ya lango la Kenya.

Taifa Stars ilizidisha kazi ya mashambulizi, ambapo dakika 38 Jonas Mkude aliachia kiki kali lakini ilitoka nje kabla ya Kenya kujibu dakika ya 39, lakini mpira wa kichwa uliopigwa na Joash Onyango ulipaa juu ya lango la Taifa Stars.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilikamilika kwa timu hizo kwenda mapumziko zikiwa nguvu sasa bila milango kufunguka.

Kipindi cha pili, Taifa Stars iliingia uwanjani na nguvu zaidi, dakika ya 58, Nado alipokea pande la Ajib na kupachika bao lakini mwamuzi alilikataa kwa madai mfungaji alikuwa ameotea.

Ajib ambaye aliingia uwanjani kuchukua nafasi ya Ayoub Lyanga alionekana kuiongezea nguvu Taifa Stars, ingawa Kenya kwa upande mwingine nayo ilionekana kujidhatiti.


Dakika 71 alishindwa kuunganisha mpira wavuni, baada ya kuanguka ndani ya kumi na nane, baada ya kupokea pasi ya Kelvin John.

Pamoja na mashambulizi ya kupokezana, dakika 90 zilikamilika kwa timu hizo kutoka suluhu.

Kocha wa Taifa Stas, Etienne Ngayiragije baada ya mchezo huo , aliwasifu wachezaji wake akisema walicheza vizuri, licha ya kutopata ushindi na kuahidi kufanya  vizuri katika mchezo wa marudiano.

Taifa Stars

Juma Kaseja, Paul Godfrey, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Kelvin Yondan, Jonas Mkude, Hassan Dilunga/ Kelvin John ,Salum Abubakar, John Bocco/ Salim Ayee, Ayoub Lyanga/IbahimAjib,Idd  Seleman

Harambee Stars

John Oyemba, Bernad Oginga, Cliffton Aisi, Joash Onyango, Mike Kibwage, Dennis Omino,Musa Masika/Ibrahim Shmabi, Whyone Isuza, Enosh Ochieng,/Pistone Mutaba, Kenneth Muguna, Duke Abuya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles