29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 28, 2024

Contact us: [email protected]

Ulega amtumbua Mkurugenzi wa Uvuvi

*Aagiza nafasi yake apewe Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Prof. Mohamed Sheikh

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ameelekeza kuondolewa katika nafasi yake Kaimu Mkurugenzi wa Uvuvi, Stephen Lukanga baada ya kushindwa kupanga na kutekeleza mikakati thabiti ya kukomesha uvuvi haramu nchini.

Waziri Ulega ametoa maamuzi hayo leo Jumanne Novemba 28, wakati akikabidhi boti (11) zenye thamani ya Sh Bilioni 1. 85 zilizotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kwa mkopo kwa wavuvi wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Waziri Ulega amefika maamuzi hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wadau wa Uvuvi mkoani Dar es Salaam ya kukithiri kwa vitendo vya uvuvi haramu katika ukanda Pwani hususan Dar es Salaam.

Oktoba 4, mwaka huu akiwa mkoani Mwanza katika Soko la Lumumba, Waziri Ulega alimtaka Kaimu Mkurugenzi huyo kuwa ndani ya mwezi mmoja ahakikishe anapanga na kutekeleza mikakati thabiti ya kukomesha uvuvi haramu nchini ambao kwa muda mrefu umekuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya sekta ya uvuvi.

Kufuatia kushindwa kutekeleza mikakati hiyo, Waziri Ulega ameamua kumuondoa katika nafasi hiyo na kuelekeza nafasi hiyo apewe aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani, Prof. Mohamed Sheikh.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles