32.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 13, 2024

Contact us: [email protected]

Uchanjaji wa mifugo nchini bado siyo wakuridhisha-

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

SERIKALI imesema suala la uchanjaji wa mifugo bado lipo nchini hivyo imepanga kushirikiana na sekta binafsi kufanya kampeni ya chanjo nchi nzima ili kuokoa mifugo hiyo.

Hayo ameeezwa leo Septemba 6, 2023 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulenga wakati akifungua mkutano wa pembeni wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) unaoendelea nchini uliowakutanisha mawaziri wa uvuvi na mifugo na wadau katika sekta hiyo wenye lengo la kuelezea fursa zinazopatika nchini katika sekta ya hiyo.

Amesema Tanzania ina fursa nyingi za Uwekezaji kwenye Sekta ya uzalishaji wa chakula cha mifugo na kuwataka wawekezaji kutoka maeneo mbalimbali duniani kuja kuwekeza kwenye eneo hilo

“Hatua hiyo itasaidia kuipa Tanzania uwezo wa kusomeka katika ramani ya dunia kuwa inauwezo wa kupambana na magonjwa hasa yanayoonekana kuwa na uwezo wa kuambukiza hata binaadamu,” amesema Ulega.

Amesema kwa upande wa ufugaji wa kisasa asilimia 100 wanafanya chanjo huku kwa ufugaji wa asili ikiwa ni asilimia 20 pekee.

Akizungumzia kuhusu malisho, Ulega amefafanua kuwa Wizara ya Mifugo, Wizara ya Kilimo na Wizara ya Fedha zote kwa pamoja zimeonyesha utayari wa Serikali katika kuhakikisha suala la upatikanaji wa malisho ya uhakika ili ng’ombe wasiendelee kufa kwa ukame.

Ameongeza kuwa hata wazalishaji wa kuku wakati wa kiangazi wanapata wakati mgumu wa malisho kwa kuwa mahindi huwa yanapanda bei sana na hivyo gharama kuongezela gharama ya uzalishaji.

Amesema wamezungumza kwa pamoja na wadau ikiwa ni pamoja na kuwapati ardhi ili wafanyekazi ya uzalishaji.

Ameongeza kuwa wao kama wasaidizi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan wameonyesha utayari wa kuhakikisha wanatatua changamoto zinazoikabili sekta ya uzalishaji nchini hasa kwa kuyaleta pamoja makundi ya vijana na akinamama katika uzalishaji.

Naye Mwekezaji Sekta ya Mifugo, Mariam Sekuwe amesema akiwa mfugaji anayemiliki ng’ombe zaidi ya 100 na mmiliki wa kiwanda cha kusindika maziwa wanayo furaha kuona jukwaa la AGRF linakuwa fursa katika kupanua wigo wa uwezeshaji wa sekta ya mifugo nchini.

Amesema upande wa masoko bado kuna changamoto na malisho kutokana na mabadiliko ya tabia nchi hivyo ni vyema wataalamu wakatumia jukwaa hilo kujadili namna ya kukabiliana na athari zilizopo.

“Nimehamasika kupitia jukwa hili kuweza kuongeza uzalishaji na kufikia soko la Afrika katika mifumo ya chakula, wizara yetu itumie nafasi hii kuwawezesha wafugaji kwa kuwapatia dawa, maabara za kisasa za mifugo na wataalamu ili kukabiliana na kupe ambao ni tishio kwa ng’ombe wengi nchini,” amesema Mariam.

Kwa upande wake Mwanzilishi wa mradi wa Malisho ya wanyama ambaye ni mnufaika wa BBT, Rogacian Njau amesema kufuatia juhudi zinazofanywa na Serikali wamepata eneo la hekari 250 Kwa ajili ya kufanya kilimo cha malisho ya wanyama.

“Tunamshukuru sana mama (Rais Dk. Samia Suluhu Hassan) kwa kutusaidia vijana hasa katika sekta ya mifugo kwani tunasaidia katika mnyororo wa thamani katika sekta ya mifugo ili mifugo iweze kupata chakula cha kutosha bila kujali hali ya hewa ndiyo maana sisi tunafanya kilimo cha malisho ya mifugo na kuhakikisha chakula cha mifugo hakikosekani muda wote,” amesema Njau.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles