30.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

Twaha Kiduku yupo fiti kumkabili mhindi

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Twaha Kiduku leo Aprili 3,2024 amewaongoza mabondia wenzake mkoani Morogoro kupima afya kuelekea pambano lake dhidi ya Hapreet Sight kutoka India.

Pambano hilo la Kimataifa lisilokuwa la ubingwa lililopewa jina la ‘Hatukimbii Hatuogopi’ linatarajia kupigwa siku ya Idd Pili kwenye ukumbi wa Tanzanite, mkoani Morogoro.

Akizungumzia maandalizi yake, Kiduku amesema amekamilisha kwa asilimia kubwa na yupo tayari kuliwakilisha vizuri Taifa kwa kuibuka na ushindi.

“Mimi pamoja na timu yangu tuko vizuri kiafya na kila kitu, naamini siwezi kuwaangusha Watanzania. Hakuna ugomvi rahisi, siku zote ugomvi ni ugomvi kikubwa ni kujiandaa na kumheshimu mpinzani,” amesema Kiduku.

Mara ya mwisho Kiduku alipanda ulingoni Desemba mwaka jana na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa pointi dhindi ya Mganda, Mohammed Sebyala, jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Mratibu wa Habari wa Peak Time ambao ni waandaaji wa pambano hilo, Victor Denis amesema kwa sasa kilichobaki ni mashabiki kuona burudani ya masumbwi kutokana na kila bondia kuwa fiti.

Mabondia wengine watakaozichapa siku hiyo ni Karim Mandonga dhidi ya Mada Maugo,Jamali Kunoga wa Marogoro kuchapana na Mrisho Mzezele wa Mbagala Dar es Salaam na mapambano mengine mengi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles