23 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Tutasimamia demokrasia – CCM

IS-HAKA OMAR-ZANZIBAR

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ amesema chama hicho kimejizatiti kutatua kero za wananchi   na kusimamia demokrasia kwa kukemea vitendo viovu vinavyohatarisha amani na utulivu wa nchi.

Kauli hiyo aliitoa katika ziara yake ya kukagua uhai na utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Jimbo la Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.

Alisema vipaumbele   ni kutekeleza kwa kasi ahadi zilizotolewa na taasisi hiyo kwa wananchi wakati wa  Uchaguzi Mkuu uliopita.

Alisema CCM kinaendelea kuaminiwa, kupendwa na kuthaminiwa na mamilioni ya Watanzania kutokana na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa sera zake  kwa kutatua changamoto za  jamii kwa wakati mwafaka.

  Dk. Mabodi alisema katika kusimamia dhana ya demokrasia, CCM haitasita kukemea vitendo viovu vinavyoonyesha  kuvunja sheria za nchi, hasa vinavyotekelezwa na baadhi ya vyama vya upinzani.

“Tumekubali kuingia katika mfumo wa vyama vingi  tushindane kwa sera na siyo kushindana kwa vituko na vurugu.

“Ni muhimu kila mwanasiasa kujitathimini juu ya mwenendo wake kwa jamii anayoiongoza,” alisema Dk. Mabodi.

Alisema zama hizi CCM mpya imekuwa ni kimbilio la wananchi wanaoamini katika siasa za maendeleo ambao wametelekezwa na vyama vyao na kupokewa  vizuri ndani ya chama hicho ili wanufaike na demokrasia iliyotukuka.

Aliwataka viongozi na watendaji wa CCM kutowawekea vikwazo wananchi wanaotaka  kujiunga na chama na badala yake wapewe fursa hiyo bila masharti magumu   na kuwasomea miongozo na itikadi za taasisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,800FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles