30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

TUPAMBANE KUTETEA DESTURI NA MISINGI YETU

NA TENGO KILUMANGA,

DIASPORA ni jamii ambayo inapenda sana kwao na asili yao. Kwani bila ya kuwa na mawasiliano, yaani bila kuwa karibu na shina lao basi madhara ni mengi. Usipofahamu na kuelewa unatoka wapi ni vigumu sana kuelewa unakwenda wapi.

Usipofahamu na kulielewa shina lako ni vigumu kuwapa vizazi vifuatavyo yako. Hasa desturi, msingi na tamaduni yenye lengo  na kuleta maendeleo ya kufika na fahamu, ambao wewe umepewa na wazazi na jamii yako. Inasikitisha  sana wakati utakuta vizazi vya leo vimepoteza malengo na kutokuelewa asili yao.

Kuelewa jinsi Watanzania tulivyokuwa katika hali mbalimbali utaona kwamba ujirani ni kuona watu wanavyoshirikiana kwenye daladala au kwenye wakati mgumu kwenye jamii. Utanzania na jinsi Watanzania wanahusiana ni jambo la msingi sana. Pale utapokuta matatizo kwenye jamii Watanzania wanashindwa.

Utulivu  na amani na nguvu inayowekwa kwenye kupata suluhisho ni moja ya  hulka yetu. Najiuliza. Sheria zetu zisitungwe kwenye misingi hiyo? Ni kitu ambacho wengi wanakielewa na pia ni kuipata jamii ya kuweza kuamua kijamii kutokana na hali na  mazingira yaliyopo. Uzito na uamuzi wa maisha ya kila siku yakiwekwa  kwenye mikono ya wanajamii basi suala la amani na usalama ni suala ambalo linawaunganisha wanajamii.

Ni sehemu ya utamaduni wetu ambao unatufanya tuweze kusaidiana na kutuwezesha kusambaza majukumu kama jamvi kwenye jamii na uzito usiangukie sehemu moja. Huu ni msingi mzuri ambao unaliwa chini tabaka tamaduni ngeni ambazo zinaua utu wetu. Safari hii niliyoanza nanyi wasomaji wangu ni ndefu na sitegemei kama itaisha leo au kesho, hata hivyo ukweli utabadilika pale pale kwamba fikra na tamaduni za kutoka nje zinaweza kuozesha zile nguvu za utamasuni wetu wa asili na kutufanya sisi kutegemea watu wengine watatue changamoto zetu.

Hakuna kitu kibaya kupata nitahangaika na kuona vilema na watu wasiojiweza wanaoomba. Ni jambo la kusikitisha,  kusaidia mmoja mmoja kama mimi binafsi nashindwa kwa sababu mita kumi ifuatayo yupo mwingine. Utamsaidia yupi na umuache nani? Kwa hiyo hapa jamvi la jamii halina uwezo wa kusaidia nje ya makazi yake. Jamvi linafanya kazi pale ulipo kwenye jami yako. Kwa sababu za tamaduni na fikra ambazo haziendani na ule utu wa  asili inafanya hawa wanaomba wanaondoka katika ile jamii ambayo inapaswa kuwasaidia.

Hali kama hii inazalisha idadi ya watu kutumia ubovu wa hili jamvi na kujitajirisha kutokujali nani unamkanyaga kwani wewe kusonga mbele kuna umuhimu kuliko wale wa pembeni yako, hakuna uelewano tena.  Upande mwingine utegemezi na tabia ya kupokea tu bila ya wewe kutafuta suluhisho na jamii yako itafanya kazi ya jamii kuwa na uzoefu na hii haileti tija katika jamii. 

Ukipanda daladala utaona jinsi watu wanavyogombania viti kwenye basi na jinsi wanavyojaa. Dereva na muuza tiketi halali nani anaumia katika safari hiyo yeye ni kujaza mpaka ukingoni hakuna kujali nani anaumia katika hali hiyo. Yote hii ni tamaa na fikra ambazo hazipaswi kuwa kwenye jamii zetu. Tusiweke maslahi yetu mbele kwanza bila ya kufikiria jamii au wengine ambao wapo kwenye hali moja.

Hali kama hii inazalisha hulka ya watu kuwa na uzoefu wa kununua nafasi ambazo wangepewa wengine  katika jamii  ninavyosema hivyo  ninamaanisha hongo ambayo imefanya kazi sana katika jamii zetu. Hii inatuumiza wote kama jamii kwani ule utu tena haupo na wengi wanaona ni haki yao kupata hiyo kwa kuwasaidia na kutoa huduma kwa wengine. Ni kweli watu husaidiana lakini tumeweka udhalimu katika huo usaidizi basi tunapoteza misingi ya utu.

Watanzania wengi nje wanaomba wapewe mfumo mzuri wa kuweza kusaidia jamii zao. Mfumo ambao unarahisisha uwekezaji na urahisishaji wao kuweza kuchangia katika maendeleo ya nchi bila ya kujali wanatoka wapi. Jamvi la jamii linapaswa kuwapoteza kwa mikono miwili kwani katika ushirikiano wetu matunda mengi yatapatikana ambayo yatarudi katika jamii tena.

Mapenzi ambayo diaspora  Watanzania inayo kwa jamii ya watanzania inathibitishwa kwa vile vitendo ambavyo jumuiya tofauti wanafanya Ughaibuni kusaidia nchi mama, mara nyingi  bila malipo. Urahisishaji wa shughuli za wanadiaspora na kuwawezesha na kuwapa miundombinu ambayo haiwakwamishi katika mazingira yanayowafanya wanashindwa kuchangia bila ya kuumiza jamii zao ughaibuni.

Hili ni suala la msingi sana kwa sababu rasilimali ambayo wanaughaibuni Watanzania ambayo wanakalia ni kubwa na kama ikiwezekana fanya uwe mipango mizuri ya kuwawezesha  kutumia nafasi zao kusaidia jamii ya Tanzania itakuwa imepata manufaa. Wanaughaibuni Watanzania wanaishi, kulala kuota na kutambua kwamba nyumbani ni nyumbani na suala ni kwamba kama nyumbani hilo hupendi linarudi. 

Ukishafahamu haya yote, basi iliyobaki ni kasi tu ya kutekeleza uliyoyalenga..

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles