23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Tume ya Haki za Binadamu yapewa somo

Na Mwandishi wetu -Zanzibar 

WAZIRI wa Katiba na Sheria wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Khamis Juma Mwalim, ameitaka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kusimamia majukumu yao kwa ufanisi kama sheria na mwongozo inavyoelekeza.

Akizungumza na ujumbe kutoka tume hiyo ofisini kwake Mazizini Unguja juzi, Mwalim alisema tume ina majukumu ya kuendeleza na kusimamia masuala ya haki na utawala bora nchini, ni vema ikasimamia kwa uadilifu zaidi.

Shimo aliahidi wizara yake kuendelea kufanya kazi na tume hiyo kwa nguvu zote.

Alisema wizara yake itahakikisha taratibu na miongozo inafuatwa katika kusimamia demokrasia, utawala bora na haki za binadamu chini ya utawala wa sheria.

“Katiba, sheria, tume kwa upande mwingine ni watoto pacha, lazima tuungane pamoja kama mihimili ili kusimamia vema majukumu ya nchi na kuendeleza amani na mshikamano wa nchi yetu,” alsema Shimo.

Naye Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji mstaafu Mathew Mwaimu alisema jukumu kubwa la tume hiyo ni kulinda, kutetea na kuhifadhi haki za binadamu nchini.

Alisema katika kutekeleza jukumu hilo, tume inayo mamlaka ya kupokea malalamiko kwa njia mbalimbali na kuanzisha uchunguzi wake endapo itaona kuna uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.

Mathew alimhakikishia  Mgumba kuwa tume itafanya kazi kwa uadilifu na kutimiza wajibu wao kwa kuzingatia taratibu na kufuata Katiba na sheria za nchi.

Kuhusu masuala ya haki za binadamu,  alisema tume hiyo ni sehemu muhimu inayosimamiwa na Wizara ya Katiba na Sheria.

Alisema ushirikiano mkubwa wa kiutendaji unahitajika ndani ya wizara inayoshughulikia masuala ya utawala bora ili kupata taarifa sahihi.

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Nyanda Shuli alisema kupitia ushirikiano huo, atatatua changamoto zitakazojitokeza na kupatiwa ufumbuzi.

Alisema tume haitaruhusu mwanya kwa baadhi ya vikundi ama taasisi kuhatarisha amani na kusababisha ukiukwaji wa haki za binadamu na utawala bora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles