24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

TTB, GNM Cargo kuwapa fursa wafanyabishara wa Tanzania kwenda China

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kushirikiana na Kampuni ya usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi ya GNM Cargo wameandaa safari ya kitalii na kibiashara kutoka Tanzania kwenda China lengo likiwa ni kufungua fursa za kibiashara na kutangaza vivutio na kuhakikisha sekta ya utalii inakua.

Akizungumza Juni 22, jijini Dar es Salaam Meneja Masoko wa TTB, Nassor Garamatatu amesema safari hiyo ni njia mojawapo ya kutangaza utalii na kukuza biashara.

“Rais Dk. Samia Suluhu amefanya juhudi kubwa kuifungua nchi na kutangaza utalii wetu kote Duniani ikiwemo Royal Tour tutumie fursa hii kuendelea kufanya utalii huu kwani umekuwa fursa kwetu kujiendeleza na kujiinua kiuchumi,” amesema Garamatatu.

Naye Mratibu wa safari hiyo, Antony Luvanda amesema itasaidia kufungua fursa kwa wananchi ambao walitamani kufanya biashara kuona fursa zilizopo China lakini pia kujua maeneo (machimbo) zinakopatikana bidhaa wanazouza.

Amesema katika safari hiyo wanategemea kupeleka Watanzania maeneo muhimu ambayo yatatoa fursa na kujifunza.

Akijata maeneo hayo kati ya maeneo watakayoenda ni pamoja na viwanda vinavyotengeneza bidhaa ambazo zinapatikana hapa nchini pamoja na masoko makubwa ya biashara.

“Tutawapeleka kwenye maeneo ambayo yatakua na fursa kubwa tuenda pia kwenye maonyesho makubwa ya biashara yanayofanyika nchini China yanayofahamika kama Canton Fair lakini pia tutaenda eneo la kitalii la Baiyun Mountain almaarufu kam Mlima Mweupe” amesema Luvunda

Aidha, Luvanda ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kuchangamkia fursa hiyo Kwani wanaweza kuanza au kukuza biashara zao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Usafirishaji GNM Cargo, Brigita Mbano amesema wao wamekuwa sehemu ya safari hiyo kwani wanauzoefu wa kutosha katika nchi ya China, hivyo watashiriki kuwaonyesha maeneo mbalimbali ya huduma ikiwemo sehemu za kufikia na machimbo ya biashara.

Safari ya kibiashara na utalii itakatofanyika nchini China ijulikanayo kam “china Business Trip na Fun Walk” inatarajiwa kuanza Oktoba 14, hadi 23,2023 huku gharama ya safari hiyo ikiwa SH million 6,242,000 ikijumuisha usafiri wa kwenda na kurudi, malazi, viingilio katika maenesho ya biashara, usafari China kwenye maeneo yote watakayotembelea, malipo ya visa ubarozini na huduma za ukarimani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles