23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Trump, Moon Jae-in waongeza vikwazo Korea kaskazini

WASHINGTON, MAREKANI

RAIS  wa Marekani, Donald Trump, ambaye jana alimpokea mwenzake wa Korea Kusini, Moon Jae-in na kufanya mazungumzo ya kina kuhusiana na masuala mbalimbali ya kidiplomasia, wakiwa Ikulu ametangaza nia yao  kufanyika mkutano mpya na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, akibainisha kwamba hana mpango wa kuondoa vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini.

Donald Trump na Moon Jae-in, ambao walizungumza katika ikulu ya White House baada ya chakula cha mchana, wamekubaliana kwa kauli moja kuwa vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitaondolewa, badala yake kiongozi huyo wa Marekani yupo tayari kufanya mkutano wa tatu na Kim Jong Un.

Viongozi hao wawili wamejadiliana uwezekano wa kufanyika mkutano huo mpya kati ya viongozi wa Korea mbili kwa lengo la kufufua mazungumzo kati ya serikali za Marekani na Korea Kaskazini.

Tangu kushindwa kwa mkutano wa jijini Hanoi nchini Vietnam mwishoni mwa Februari mwaka huu, majadiliano kati ya Marekani na Korea Kaskazini yamesimama. Kabla ya ziara ya Moon jijini Washington, washauri wake walisisitiza haja ya kuanzisha tena majadiliano hayo.

“Mkutano wa tatu (pamoja na Kim Jong-un) unaweza kufanyika. Tunakwenda hatua kwa hatua. Si mchakato wa kufanyika haraka, sijawahi kusema kuwa jambo hilo litakuwa au halitakuwa,” Trump alisema katika mazungumzo yake na vyombo vya habari.

Aliongeza kuwa, mambo mazuri yalitokana na mazungumzo na Korea Kaskazini, ingawa hakupata kile alichotaka katika mikutano yake miwili ya kihistoria na Kim Jong Un Juni 12 mwaka jana nchini Singapore, kisha Februari 27 na 28 jijini Hanoi nchini Vietnam.

Wakati huo, kumekuwa na hali ya sintofahamu kuhusiana na iwapo kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un anatafakari kujitoa kutoka katika majadiliano ya kinyukilia ama kuanza tena majaribio ya makombora.  

Lakini Trump amesema ana uhusiano mzuri na Kim Jong Un na hakuondoa uwezekano wa mkutano wa tatu, ama kuchukua hatua kupunguza upungufu wa chakula na mahitaji mengine nchini Korea Kaskazini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles