26.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

TRUMP AMPONGEZA UHURU, RAILA KUTANGAZA UAMUZI LEO

WASHINGTON, MAREKANI

RAIS wa Marekani, Donald Trump, amempongeza Rais Uhuru Kenyatta kwa ushindi aliopata katika uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne wiki iliyopita nchini Kenya.

Taarifa rasmi kutoka Ofisi ya Katibu wa Mawasiliano wa Utawala wa Trump, imesema Marekani imefurahishwa na ushindani ulioonekana katika uchaguzi huo.

Aidha aliipongeza Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) na Wakenya kwa ujumla kwa kuendeleza shughuli hiyo ya uchaguzi kwa njia ya ‘haki, huru na ukweli’.

Taarifa hiyo inasema kuwa Trump ameridhika na taarifa za waangalizi wa uchaguzi, ambao waliteuliwa kushuhudia tukio hilo.

Tayari kinara wa Muungano wa upinzani wa National Super Alliance (Nasa), Raila Odinga, aliyeibuka wa pili kwa kuzoa asilimia 44 ya kura halali zilizopigwa, amekataa kukubali matokeo, akidai uwapo wa wizi mkubwa wa kura, hasa katika majumuisho.

Hata hivyo, ameonekana kutengwa na wadau wengi katika taifa hilo na wa kimataifa, ambao wanaonekana kukubaliana na mchakato ulivyoenda.

Hata hivyo, Trump alieleza masikitiko yake kwa maandamano ya hapa na pale yaliyoshuhudia ghasia na vifo.

Amemtaka yeyote ambaye hajaridhika na matokeo atumie njia mbadala ambazo zimewekwa kikatiba.

Trump amewataka Wakenya wadumishe amani na umoja, akisema hiyo ndiyo njia ya kipekee ya kusaka ufanisi wa kimaisha na maendeleo.

Ameihakikishia Kenya kuwa Marekani itaendelea kuwa mshirika wa karibu kwa Wakenya na kusaka manufaa halisi kwa raia.

Wakati Wakenya wakielekea uchaguzini, kulikuwa na taswira miongoni mwa wafuasi wa Jubilee kuwa huenda Marekani ilikuwa ikimuunga mkono Raila, huku wengine wakimfananisha Trump na kinara huyo wa chama cha ODM.

Hata hivyo, Marekani imekuwa ikikana madai hayo, ikisema haikuwa ikiunga mkono mrengo wowote wa kisiasa.

RAILA KUTANGAZA HATUA ATAKAYOCHUKUA LEO

Katika hatua nyingine, Nasa imeahirisha kikao cha kutoa tangazo kuhusu mweleko wa chama hicho baada ya uchaguzi.

Kiongozi wa muungano huo, Raila, Jumapili iliyopita alihidi kuwa jana angetangaza hatua gani atachukua baada ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa Ijumaa iliyopita.

Wakala mkuu wa Nasa wakati wa uchaguzi wa urais, Musalia Mudavadi, amesema sasa muungano huo umepanga kutoa tangazo leo.

“Tunasikitika kwamba mashauriano ndani ya NASA yanachukua muda mwingi kuliko ilivyotarajiwa, kwa hiyo hawataweza kuwahutubia Wakenya kama ilivyotarajiwa leo (jana).”

Awali Raila aliwataka wafuasi wake kususia kazi, lakini hata hivyo wito huo haukuitikiwa kwa wingi baada ya wengi kuonekana kuupuuza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles