25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

TPA kujenga bandari kavu Moshi, Arusha

Janeth Mushi, Arusha

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), iko mbioni kujenga bandari kavu ya muda mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, kwa ajili ya kuhifadhi makontena yanayotoka nje ya nchi hususani  kahawa inayotoka Arusha na Kilimanjaro kwenda nje ya nchi yatahifadhiwa hapo.

Aidha, Bandari Kavu ya Arusha itajengwa eneo la Malula wilayani Arumeru ambapo mizigo yote itahifadhiwa hapo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe leo Alhamisi Februari 27, jijini Arusha alipokuwa akikagua ukarabati wa reli hiyo yenye urefu wa kilomita 86 kutoka Moshi hadi Arusha.

“Wakati wowote kuanzia sasa TPA itajenga  bandari ya muda ambayo itahifadhi mizigo kutoka ndani na nje ya nchi.

“Lakini ndugu zangu mnajua kuna abiria wengi kutoka Moshi-Arusha… tunakaa kikao tukubaliane kwa kushirikisha na sekta binafsi tununue treni za abiria zilizo nzuri ambazo zitafanya kazi kati ya Moshi na Arusha saa 24, zilizo safi zenye AC, kamuziki ndani ikiwezekana na ndafu ndani,” amesema Kamwelwe.

Naye Mhandisi wa Reli anayesimamia ukarabati huo kuanzia Tanga, Shadrack Massawe, amesema ukarabati wa reli hiyo uko katika hatua za mwisho na umekamilika kwa zaidi ya asilimia 94.

“Ukarabati  unaendelea uko katika hatua za mwisho, zimefanyika kazi nyingi ikiwamo kurudishia matuta, reli zilizokuwa zimeibwa, tumejenga madaraja makubwa saba, madogo 30 na mengine tukarudishia mataruma.

“Kazi inayoendelea upandishaji daraja kwa njia hii ambayo ilikuwa ya reli ndogo ya paundi 45 na sasa hivi tunatandika kwa kutumia paundi 60 na tumeshafikia asilimia 38 hadi sasa hivi katika kutandika kwa kutumia paundi kubwa,” amesema.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles