23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

TMA: WANANCHI WACHUKUE TAHADHARI

Na Mwandishi Wetu,

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewatahadharisha wananchi kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi na TMA, mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24 inatarajia kuendelea kusambaa katika maeneo mengi nchini.

TMA ilisema mvua hizo zitaendelea kunyesha hadi leo katika baadhi ya mikoa.

Mikoa inayotarajiwa kuathirika na mvua hizo kubwa ni Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Tanga, Pwani na Morogoro pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba.

“Wakazi wa maeneo yaliyotajwa wanashauriwa kuchukua tahadhari na hatua stahiki,” ilisema taarifa hiyo.

TMA ilisema mvua hizo zinatokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua nchini.

Mwezi uliopita, Serikali ilitoa maagizo kwa wananchi wanaoishi maeneo ya mabondeni, hasa Mto Msimbazi, Mkoa wa Dar es Salaam, kuhama mara moja kuepuka maafa ambayo yanaweza kutokea.

Kila mara mvua kubwa inaponyesha husababisha mafuriko makubwa kutokana na miundombinu ya Jiji la Dar es Salaam kushindwa kumudu.

Mathalani licha ya jana mvua kunyesha kwa muda mfupi majira ya asubuhi, gazeti hili lilipita katika maeneo kadhaa na kukuta maji yakiwa yametuhama.

Katika eneo la kuegesha mabasi ya mwendo kasi, Jangwani, kulikuwa na maji yaliyotuhama ndani na nje ya kituo hicho na eneo la viwanja vya Jangwani na kusababisha kusimamishwa kwa baadhi ya shughuli za wakazi wa eneo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles