29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

Timu Angola, Kongo kucheza Kagame

Timu ya Vital’O ya Burundi
Timu ya Vital’O ya Burundi

Na Abducado Emmanuel, Dar es Salaam

BARAZA la Vyama vya Soka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), linatarajia kuzialika timu kutoka Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Kongo Brazzaville, kushiriki michuano ya Kombe la Kagame yanayotarajia kuanza Agosti 9 hadi 23 mwaka huu jijini Kigali, Rwanda.

Bingwa mtetezi wa michuano hiyo ni Vital’O ya Burundi, ambapo hushirikisha timu ambazo ni mabingwa wa ligi za nchi wanachama wa CECAFA, pamoja na timu kadhaa ambazo hualikwa nje ya ukanda huu, ili kunogesha mashindano, Yanga SC inatarajia kuiwakilisha Tanzania katika Kagame.

Akizungumza kupitia mtandao wa ‘Cafonline’ Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye, alisema jumla ya timu kutoka nchi hizo zinatarajia kuungana na mabingwa wa nchi wanachama wa CECAFA, kushiriki michuano hiyo.

“Timu nne kutoka Angola, DRC na Congo Brazzaville tunatarajia kuzialika kushiriki michuano hiyo inayodhaminiwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame ambaye hutoa kiasi cha Dola za Kimarekani 60,000 kwenye michuano hiyo tokea mwaka 2002,” alisema Musonye.

Katika hatua nyingine, Musonye alimpongeza Rais Kagame, kwa kukubali kushirikiana na CECAFA, huku akidai kwa mwaka huu itakuwa ni michuano bora zaidi kutokana na maandalizi makubwa yaliyofanywa na CECAFA, Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) na Wizara ya Michezo na Utamaduni ya Rwanda.

“Rwanda ipo tayari, CECAFA tupo tayari na timu zote zipo tayari kuja kushiriki michuano hiyo. Tunatarajia kuwa na timu nyingi za kushiriki mwaka huu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles