30.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 10, 2024

Contact us: [email protected]

TFS kuimarisha mifumo ya Ikolojia

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imesema katika kuhakikisha nchi inapata bidhaa bora zitokanazo na zao la misitu itaimarisha mifumo ya Ikolojia nchini ili iweze kutoa hewa safi, maji na makazi bora ya wanayamapori.

Akizungumza Julai 8, jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari baada ya kutembelea mabanda yaliyopo kwenye maonyesho ya 47 ya biashara ya kimataifa maarufu sabasaba Kamishina wa Uhifadhi wa TFS, Profesa Dos Santos Silayo amesema TFS imepewa wajibu wa kuhakikisha nchi inapata bidhaa bora zitokanazo na zao la misitu.

Amesema zao la misitu ni muhimu ambalo hutumika kwenye maendeleo ya taifa kuanzia bidhaa za ujenzi, Nishati zinazotokana na mimea hiyo na kuongeza PatolaTaifa.

“TFS imekuwa ikishirikiana na Serikali katika upandaji miti ili kuongoa maeneo yaliyoharibika, kuonesha uwekezaji katika maeneo ya viwanda na miaka ya hivi karibuni tumeweza kuongeza kiwango cha uwekezaji wa ndani na kusafirishaji zaidi mazao ya misitu kuliko ilivyokuwa awali, amesema miaka mitano iliyopita walikuwa na (Q³) 25,000 kwenda nje ya nchi na kuingiza Q³,”amesema Profesa Silayo.

Akizungumzia sekta ya ufugaji Nyukia, Profesa Silayo amesema kuwa wanaendelea kuhamasisha wananchi kujihisisha na ufugaji nyuki, Uchakataji wa zao la nyuki, kuboresha mnyororo mzima wa thamani pamoja na usafirishaji katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

“Tumepata masoko makubwa nje ya nchi, Sasa ni wajibu wa wadau wetu wa ndani wanaofanya biashara za kimataifa kuyakaribia masoko hayo na kufanya biashara ya kimataifa pamoja na kuwezesha nchi kupata fedha za kigeni,” amesema Prof. Silayo.

Amesema ufugaji wa nyuki wanaupa kipaombele kwani kuna masoko ambayo yameshafanyiwa tathmini za ubora wa zao la nyuki nchini na zinakidhi vigezo vya uuzaji kwenye masoko ya nje ya nchi.

Amesema kuwa kumekuwa na mageuzi makubwa katika uwekezaji hapa nchini hasa ukiangalia viwanda vilivyowekezwa vimeleta teknolojia ambazo hazikuzoeleka hapo kabla.

Amewaasa kuzalisha bidhaa zenye ubora wa viwango vya juu ili wasije kuharibu masoko, lakini wazalishe kwa kiwango kikubwa kwani kwa sasa kiwango ni kidogo

Aidha, amewaalika wadau mablimbali kutembelea banda lao ili waweze kupata elimu juu ya uwekezaji kwenye sekta mbalimbali zinazosimamiwa na TFS.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles