24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

TAWA yakutana na wakuu wa wilaya zinazozunguka pori la akiba Kilombero

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imekutana na kufanya kikao na viongozi mbalimbali wanaolizunguka Pori la Akiba Kilombero Februari 23, 2023 mkoani Morogoro.

Kikao hiko kililenga kujadili shughuli za uhifadhi wa Pori la Akiba Kilombero na kupanga mikakati ya ushirikiano katika utekelezaji wa Tangazo la Serikali Na. 64 lililoianzisha Pori la Akiba Kilombero.

Tangazo hilo lilitolewa 17 Februari, 2023 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan.

Kikao hicho kilijumuisha, Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Sebastian Waryuba, Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Julius Ningu na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Dunstan Kyobya.

Wengine waliohudhuria kikao hiko ni Wakurugenzi wa Wilaya za Mlimba na Ulanga pamoja na Makatibu Tawala wa Wilaya za Ulanga, Malinyi na Kilombero.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles