25.9 C
Dar es Salaam
Friday, December 13, 2024

Contact us: [email protected]

TAPA yaunda Kamati ya mabadiliko

Na Victoria Godfrey, Dar es Salaam

Chama cha Pool Table Tanzania (TAPA) kimefanikiwa kuunda Kamati ya Mabadiliko ya kufufua na kuendeleza mchezo huo hapa nchini.

Kamati hiyo iliundwa katika Kikao cha wadau wa mchezo huo kilichofanyika Jumapili iliyopita jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na www.mtanzania.co.tz , Mwenyekiti wa TAPA, Isack Togocho, amesema Kamati hiyo itakuwa na majukumu yakuahkikisha mchezo huo unarejesha heshima kama awali.

Alitaja majukumu ya kamati hiyo ni kuongeza hamasa mchezo, kutengeneza Kamati mbalimbali za Chama, kuhamasisha Uchaguzi kuanzia ngazi ya mkoa na Taifa.

Togocho amesema majukumu mengine ni kuhamasisha vilabu na chama vinalipa ada ya chamani na Taifa na uanzishwaji wa ligi ngazi mbalimbali.

Kamati hiyo imeundwa na Isack Togocho, Amos Kafwinga, Mafco Magege, Salehe Amin, Cesy Kileo, Mohamed Mwarabu, Ibrahim Kaburu, Shedrack Pascal na Omari Hatibu Omari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles