30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

TANZANITE YAUZWA GHALI ZAIDI KWA MIEZI MITATU

Maregesi Paul, Dodoma

Waziri wa Madini, Angela Kairuki amesema madini ya Tanzanite yameuzwa kwa fedha nyingi kwa kipindi cha miezi mitatu kuliko yalivyouzwa katika kipindi cha miaka mitatu.

Taarifa hiyo imetolewa bungeni jijini Dodoma leo Mei 31, na waziri huyo alipokuwa akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/19.

“Kwa miezi mitatu kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu, wizara imekusanya mrabaha wa Sh milioni 714.6 na katika kiasi hicho Sh milioni 614.6 zinatokana na makusanyo kutoka kwa wachimbaji wadogo.

“Katika mwaka 2015 tulikusanya mrabaha wa Sh milioni 166.8, mwaka 2016 mrabaha wa Sh milioni 71.8 na mwaka 2017 Sh milioni 147.1 kutoka kwa wachimbaji wadogo,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Kairuki amewataka wamiliki wa leseni za madini kuacha tabia ya kukwepa au kuchelewa kulipa kodi, kulipa mrabaha na tozo nyingine kwani watakaobainika walikiuka sheria za shughuli zao watafutiwa leseni na kufikishwa mahakamani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles