30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 30, 2023

Contact us: [email protected]

TANZANIA YASEMA ILIMUUNGA MKONO AMINA MOHAMMED WA KENYA

Tanzania imepuuzilia mbali madai kwamba baadhi ya mataifa ya Afrika Mashariki hayakumpigia kura mgombea Amina Mohammed wa Kenya katika uchaguzi wa mwenyekiti wa Muungano wa Afrika.

Amina ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, alishindwa na mwezake wa Chad Moussa Faki Mahamat, ambaye sasa ni mwenyekiti wa AU.

Akizungumza na BBC jijini Addis Ababa, Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Augustine Mahiga, amesema madai katika baadhi ya vyombo vya habari nchini Kenya kuhusu uchaguzi huo ni ya kupotosha.

Awali, mgombea wa wadhfa wa mwenyekiti kutoka Kenya katika tume ya Umoja wa Afrika AU Amina Mohammed alitaja usaliti miongoni mwa mataifa jirani ya Afrika Mashariki kuwa sababu ya yeye kutoshinda wadhfa huo.

Balozi Amina alilaumu kushindwa kwake kulitokana na uwongo wa majirani za Kenya na siasa zinazoendelea kati ya mataifa yanayozungumza Kifaransa Francophone na wale wanaozungumza kizungu Anglophone.

Akiongea na vyombo vya habari vya kimataifa mjini Addis Ababa Amina alisema kuwa alipoteza wadhfa huo kutokana na usaliti wa majirani za Kenya ambao walikuwa wameunga mkono harakati zake. Chanzo BBC

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles