23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania ya mwisho viwango vya furaha duniani

happy-people2Na Mashirika ya Habari

TANZANIA ni miongoni mwa nchi 10 za mwisho kwa viwango vya furaha duniani.

Hiyo ni kwa mujibu wa Ripoti ya Viwango vya Furaha duniani ya 2016 ambayo ilitolewa   Rome, Italia jana wakati dunia ikijiandaa kuadhimisha Siku ya Umoja wa Mataifa ya Furaha Duniani  Machi 20.

Nchi nyingine ambazo zimo kwenye kundi hilo  ni Madagascar, Liberia, Guinea, Rwanda, Benin, Afghanistan, Togo, Syria ,huku Burundi ikishika mkia.

Taarifa iliyotolewa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) jana, ilisema orodha hiyo iliandaliwa kwa kuzingatia pato la mtu kila mwaka.

Mambo mengine yaliyozingatiwa ni  miaka ambayo mtu anatarajia kuishi, mtu wa kutegemea kwa usaidizi, dhana ya kuwapo uhuru wa kufanya uamuzi, uhuru kutoka kwa ufisadi na ukarimu katika jamii.

Takwimu zinaonyesha Tanzania imeshika  namba 149 kati ya nchi 157, ikiwa na alama 3.695 kati ya alama 10 na Rwanda ni ya 152 ikiwa na alama 3.315.

Uganda ni namba 146 na alama 3.739, Malawi ya 132 na alama 4.156, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imeangukia namba 125, ikiwa na  alama 4.272, wakati  Kenya imeshika  namba 122 ikiwa na alama 4.356 na Somalia ndiyo kinara kwa kuwa namba 76 ikiwa na alama 5.44.

Orodha hiyo  imetayarishwa na Shirika la Maendeleo Endelevu la Sustainable Development Solutions Network (SDSN) ambalo lilianzishwa na Umoja wa Mataifa.

Nchi 10 bora zinaongoza kwa furaha duniani  ni Denmark  ikiwa na alama 7.526  ikifuatwa na Uswisi, Iceland na Norway.

Nyingine ni Finland, Canada, Uholanzi, New Zealand, Australia na Sweden zinafunga 10 bora.

Ripoti hiyo imeonyesha Marekani inashika nafasi ya 13 duniani  wakati Uingereza ipo nafasi ya 23.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles