24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

TANZANIA SEHEMU SALAMA YA UTALII -BENKI YA DUNIA

WASHINGTON, MAREKANI


HATUA ya kuongezeka kwa uhifadhi na usimamizi wa maeneo ya pekee ya Kusini mwa Tanzania na kukuza viumbe mbadala kwa jamii   vijijini na maendeleo ya miundombinu, kunatajwa kama sababu za kuwa sehemu salama kwa utalii nchini.

Pia inaelezwa kwamba hali hiyo itachangia kuweapo   fursa za  uchumi kwa kanda, kulinda mali ya asili  ambako kaya zaidi ya 40,000 zinaweza kufaidika na fursa hizo.

Hayo yalisemwa   jijini Washngton, Marekani na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa   Tanzania, Malawi, Somalia na Burundi, Bella Bird.

Alikuwa  akitangaza matokeo ya utafiti kwa kipindi cha miaka sita ijayo kupitia mkopo wa Dola milioni 150 zilizotolewa na Chama cha Kimataifa cha Maendeleo kwa njia ya Usimamizi wa Rasilimali za Utalii na mradi wa Kukuza Uchumi (Regrow),  uliopitishwa Septemba 28, mwaka huu na Benki ya Dunia.

“Lengo la Regrow ni kuboresha usimamizi wa rasilimali za asili na mali za utalii katika maeneo ya kipaumbele ya Kusini mwa Tanzania na kuongezeka shughuli za uendeshaji mbadala kwa jumuiya husika,” alisema Bird.

Alisema  pia kuwa itasaidia kukuza uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa na mbuga za wanyama, kupunguza mgogoro kati ya binadamu na wanyamapori na kuimarisha ustahimilivu wa mazingira magumu na mabadiliko na kuchangia kwenye mtiririko wa ulinzi kutoka Mto Ruaha kwenda kwenye Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

“Utalii ni kipengele muhimu cha uchumi wa Tanzania na ulichangia kwa asilimia 10 ya Pato la Taifa mwaka 2015.

“Nchi hii imepewa viumbe hai na vivutio vya wanyamapori, lakini watu wengi wanafahamu zaidi vivutio vilivyopo Kaskazini mwa Tanzania.

“Vivutio vilivyopo Kusini vinaweza kuongeza idadi ya watalii   nchini na hivyo kuongeza faida za  uchumi na kukuza uhifadhi wa wanyamapori. Ili iwe hivyo, miundombinu na huduma zinahitajika kuboreshwa,” alisema Bird.

Alivitaja vivutio vilivyopo Kusini mwa Tanzania kuwa ni Hifadhi za Katavi, Kitulo, Mahale, Milima ya Udzungwa, Mikumi na Ruaha na vivutio vinginevyo kama mbuga ya Selous, maziwa ya Nyasa na Tanganyika na vinginevyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles