23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania ni kinara utoaji fedha za utafiti-COSTECH

Na Asha Bani, Mtanzania Digital

NCHI ya Tanzania ni ya kwanza katika kutoa fedha za utafiti ikifuatia nchi ya Afrika Kusini katika nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Hayo yalielezwa jana na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk. Amos Nungu katika kikao cha kujenga mahusiano mazuri na waandishi wa habari kilichoandaliwa na tume hiyo.

Alisema Tanzania ndio ya kwanza katika kusimamia na kuratibu utafiti, kikiwepo kutoa miongozo mbalimbali ya utafiti, kusimamia fedha na kuangalia tafiti zinazoweza kupelekwa kwa jamii.

Alibainisha kua kutokana na kusimamia vizuri wapo wanaotaka kujifunza Tanzania na tayari nchi ya Namibia iko tayari kuja kujifunza sambamba na Ghana.

Naye Mkurugenzi wa Uratibu na Uendelezaji wa Utafiti COSTECH, Dk Bugwesa Katale alisema Tume hiyo ni mwanachama wa mabaraza ya utafiti wa nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Alisema COSTECH imekuwa ikifadhili tafiti na bunifu mbalimbali ambazo zinatoa teknolojia chanya kwa taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles