23.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Tanzania Marine yawafariji waogeleaji Olimpiki

kaoge

NA WINFRIDA NGONYANI, DAR ES SALAAM

KLABU ya kuogelea ya Tanzania Marine (TMSC), imewataka waogeleaji watakaokwenda kuiwakilisha Tanzania katika michezo ya Olimpiki kuendelea kujifua.

Mkurugenzi wa TMSC, Geofrey Kimimba, aliliambia MTANZANIA jijini Dar es Salaam jana kuwa wao kama waogeleaji wanaitakia mafanikio mazuri timu ya kuogelea ya Tanzania na kuwataka kutokata tamaa juu ya safari yao.

“TMSC kwanza tumefurahishwa na kitendo cha kupata waogeleaji ambao watakwenda nchini Brazil kutuwakilisha, hivyo kwa namna ya kipekee tungependa kuendelea kuwatakia maandalizi mema ya Olimpiki, vile vile tukiwataka kuacha kukata tamaa kwani Serikali inatambua mchango wao,” alisema Kimimba.

Tanzania inawakilishwa na waogeleaji; Hilal Hemed Hilal na Magdalena Ruth Alex, ambao wamepata nafasi ya upendeleo wakiogelea mita 50 ya mtindo wa ‘freestyle’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,718FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles