27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, December 3, 2023

Contact us: [email protected]

Tanesco: Hatuingii tena mkataba na Symbion, Agreeko

tanescologoNa Humphrey Shao, Dar es Salaam
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), limesema halitaongeza mkataba na Kampuni ya kufua umeme ya Agreeko na Symbion kutokana na kukamilika kwa asilimia 72 mtambo wa kuzalisha umeme wa gesi wa Kinyerezi 1.
Uamuzi huo, ulielezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Dk. Mighanda Manyahi, baada ya kumaliza ziara ya kutembelea mtambo wa Kinyerezi 1 na vituo vingine vidogo vya uzalishaji umeme Mkoa wa Dar es Salaam jana.
“Kituo hiki kikimalizika kitaweza kutoa megawati 150, hakuna sababu ya Tanesco kuendelea kutumia mitambo ya kukodi ya Symbion na Agreeko ambayo inatumia fedha nyingi na gharama kubwa kuelemea wananchi,” alisema Dk. Manyahi.
Mbali na kufuta mikataba, pia Tanesco haitaendelea kutumia mitambo ya kukodi ya umeme wa dharura pindi mradi wote wa Kinyerezi utakapokamilika, kwani utaweza kufanya kazi kwa kipindi chote na kutosheleza mahitaji ya nchi nzima.
Hata hivyo, Dk. Manyahi alisema ujenzi wa vituo vya kuzalishia umeme una changamoto kutokana na migogoro ya viwanja katika maeneo ambayo shirika limeweka miundombinu yake.
Naye Meneja Mradi wa Kinyerezi, Mhandisi Simon Jilima, alisema mtambo huo unatumia njia mbili; ya gesi na mafuta, hivyo utafanya kazi saa zote hata kama kukiwa na tatizo la gesi hapa nchini.
“Mtambo huo una njia mbili za kuingiza chanzo cha nguvu… njia ya gesi itafanya kazi muda wote huku ile ya mafuta itatumika wakati Shirika la Maendeleo la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), litakapokuwa linafanya usafi katika bomba lake,” alisema Jilima

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles