24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

TAMISEMI ‘kupiga chini’ Wakurugenzi watakaosuasua kwenye mapato

Na Safina Sarwatt,Arusha

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Angellah Kairuki amesema wakurugenzi wa halmashauri ambao watashindwa kufikia malengo ya ukusanyaji mapato, watapigwa chini.

Kairuki ameyasema hayo leo Juni 1, 2023 wakati akifunga Mkutano Mkuu wa 37 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika jijini Arusha.

Kairuki amesema baadhi ya halmashauri nchini zikiongozwa na Jiji la Dar es Salaam, Manispaa ya Kinondoni na Ubungo, wameshindwa kutoa leseni za biashara kwa wahitaji, na kusema jambo hilo linaweza kukosesha mapato kwa halmashauri.

“Tutapataje pesa kama hatutoi leseni. Halmashauri haiwezi kupata mapato kama hakuna watu wanaofanya biashara na baadhi ya halmashauri ikiwemo Jiji la Dar es Salaam hawatoi leseni kwa baadhi ya wafanhabiashara wanaohitaji leseni hizo. Mkurugenzi ambaye atashindwa kufikia malengo ya ukusanyaji mapato hatavumilika,” amesema Kairuki.

Amesema, baadhi ya halmashauri hazipeleki benki fedha mbichi jambo hilo linasababisha halmashauri kupata matatizo ikiwemo hoja za ukaguzi, na kuagiza fedha zote mbichi zipelekwe benki, na kuongeza kuwa Mfumo wa Tausi utakuwa mkombozi kwa tatizo hilo.

Kairuki amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kufanyakazi na madiwani kwa mahusiano mazuri ili kuona fedha zinazopelekwa kwenye halmashauri zinasimamiwa na watu wanaoshirikiana, huku kila mmoja akiheshimu mipaka na wengine.

Akizugumzia mashine za ukusanyaji mapato (Posi) amesema kuwa halmashauri 10 zimeonekana kuzima posi kwa muda mrefu, ikiwemo Mbeya Jiji posi 124, Dodoma Jiji posi 121, Temeke posi 95, Kinondoni posi 88,Tunduma posi 84, Iramba posi 81, Dar es Salaam Jiji posi 77, Mbarali posi 74, Makete posi 72 na Muleba posi 72.

“Hizi ni halmashauri chache tu 10 ambazo nimezitaja na siyo kwamba wengeni hawazimi posi hivyo basi naomba niwambie kwamba kila mmoja awajibike kwasababu suala hili halitavumilika nendeni mkajipange,”amesema Kairuki na kuongeza kuwa:

“Unapokuwa kiongozi na wewe mwenyewe ukakosa maadili kwa kweli mnajiweka katika mazingira mbaya nendeni mkafanye kazi mkaheshimiane,kila moja akajua mipaka yake ya kazi,”amesema.

Katika hatua nyingine amezitaka halmashauri kuwa na vikusanyia taka kwenye miji yote ili kupunguza malalamiko ya wananchi kuwa taka zinazozalishwa hazikusanywi kwenye maeneo ya shughuli za kijamiii kabla ya kwenda kutupwa dampo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles