23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Takukuru yawafikisha sita mahakamani kwa uhujumu Uchumi

Faraja Masinde

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, leo Jumatano Novemba 20, imewakamata na kuwafikisha mahakamani wafanyabiashara sita wakiwamo raia wa kigeni kutoka nchini China kujibu mashtaka ya Rushwa na uhujumu uchumi.

Kaimu Mkurugenzi wa Uchunguzi), Wli Mfuru amewataja watuhumiwa hao waliofikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha mkoani Pwani kuwa ni You Hattao, Zhang Zhi Xin wote raia wa China, wengine ni John Mnyele, Loncolin Ilungu, Andrew Kowelo na Emmanuel Maro, ambao wote ni watanzania.

Watuhumiwa hao wote kwa pamoja wanashtakiwa kwa makosa saba.

Amesema kuwa uchunguzi uliofanywa na Takukuru na Jeshi la Polisi umebaini kuwa kampuni ya SHIN UP iliyopo Visoga-Kibaha imejihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na uhujumu uchumi na hivyo kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh Bilioni 1.2.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,636FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles