25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Takukuru yarejesha mashamba, fedha Kilimajaro

Na Upendo Mosha,Moshi

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kilimanjaro, imerejesha mashamba yenye ukubwa wa ekari 10 na Viwanja Vitatu, vyote vikiwa na thamani ya Sh milioni 74 ambavyo ni mali ya watoto wanne wa marehemu Akida Masiki.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari, Mei 7, 2021 Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kilimanjaro, Frida Wikes, amesema mashamba na viwanja hivyo vipo katika kata ya Kahe wilaya ya Moshi vilivyokuwa vimetwaliwa na Baba yao Mdogo aitwaye Hassan Masiki.

“Hassan Masiki aliteuliwa na Ukoo kuwa Msimamizi wa Mirathi na hivyo kutenda makosa kinyume na sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2017 ya kujitwalia shamba hilo kinyume cha sheria.

“Watoto hao walipokuwa wakidai mali za urithi kutoka kwa baba yao mdogo alikuwa akiwazungusha kuwagawia na kuwafungulia malalamiko ya uwongo kwenye vituo mbalimbali vya polisi ili wasiendelee kudai haki zao ikiwa ni pamoja na kughushi baadhi ya nyaraka ili kihalalisha umiliki wake kimabavu,” alisema Farida.

Aidha, Farida amesema baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu, watoto hao ambao ndio wamiliki halali walifika katika Ofisi ya Takukuru kituo maalumu cha Holili ambapo uchunguzi ilifanyika na ikabainika kuwa msimamizi huyo wa mirathi kwa kushirikiana na ndugu wengine alikuwa na lengo la kutaka kujimilikisha mali zote za marehemu kaka yao bila kuwapatia chochote watoto wa marehemu.

Amesema baada ya uchunguzi kukamili watoto hao walirejeshewa mali zao zote mbele ya viongozi wa vijiji ambapo ni pamoja na mashamba hayo yenye ukubwa wa hekari 10 na viwanja vitatu.

Wakati huohuo Taasisi hiyo, imefanikiwa kurejesha hati ya Nyumba, yenye thamani ya Sh milioni 150 mali ya  Mjane Martha Eliza Fadhili, ambayo iliongezewa jina na mmiliki mwenza, ambaye si mwanafamia.

Amesema Mjane huyo na mumewe, walikuwa wakiishi nchini Canada na kuipangisha nyumba hiyo kwa mpangaji waliyemuamini ambaye alienda kuongeza jina kwenye hati ya umiliki bila wao kujua.

“Mpangaji huyo waliokuwa wakimuamini, aligushi nyaraka na saini na kwenda kuongeza jina lake kwenye hati ya umiliki wa kiwanja hicho bila wao kugundua, lakini baada ya Takukuru kufanya uchunguzi, tulibaini kosa hilo na kumjulisha msajili wa hati ambaye alifuta hati iliyokuwa imegishiwa na kutoa hati nyingine kwa Mjane Martha,” alisema Farida.

Katika hatua nyingine, Takukuru imefanikiwa kurejesha Sh milioni 1.3 kwa Mabuni aliyekuwa akisambaza mahindi ya chakula katika shule ya msingi Magereza.

“Mkuu wa shule ya Msingi Magereza, alikuwa akimzungusha kumlipa Mzabuni fedha hizo, tangu mwaka 2017 baada ya kusambaza chakula, ambapo alikuwa amezitumia kwa matumizi yake binafsi, kinyume cha sheria,” alisema Farida.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles