33.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 19, 2021

Takukuru yabaini ubadhirifu wa milioni 500/- Ileje

 IBRAHIM YASSIN -SONGWE

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Songwe, imefanikiwa kuokoa zaidi ya Sh milioni 500 zilizofanyiwa ubadhirifu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijamii.

Taasisi hiyo pia imeshangazwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje kushindwa kuwalipa madiwani zaidi ya Sh milioni 40 ikiwa ni malimbikizo ya posho za vikao vya miezi nane.

Akizungumza jana na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Takukuru mkoani Songwe, Damas Suta alisema fedha hizo zimetokana na vyama vya ushirika (AMCOS) ambazo wanachama au viongozi wa vyama vya ushirika walikopa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB).

Alisema baada ya wanachama hao kukopa fedha hizo hawakuweza kurejesha na badala yake walizitumia katika matumizi mengine na kwamba fedha zingine zilizookolewa ni za makusanyo ya ndani za Halmashauri za Mbozi, Tunduma, Ileje na Songwe.

Alisema baadhi ya watendaji walipewa dhamana ya kukusanya mapato kwa kutumia mashine za (PoS), ambapo baada ya kukusanya hawakuziwakilisha fedha hizo benki.

Kamanda Suta alizitaja fedha za ushirika katika halmashauri kuwa ni Wilaya ya Songwe ziliokolewa Sh milioni 29.5, Ileje Sh milioni 3.2, Momba Sh milioni 36.7 jumla kuu ni Sh milioni 69.5, wakati fedha za mapato ya ndani, Mkoa wa Songwe Sh milioni 2.3,Tunduma ni Sh milioni 707, Wilaya ya Songwe Sh milioni 10.8 ambapo fedha zilizodhibitiwa ni Sh milioni 308.

Alisema fedha zilizookolewa kwenye mradi wa maji taka ni Sh milioni 297.9,ujenzi ofisi ya mkoa ni Sh milioni 42.2, ujenzi hospitali ya rufaa mkoa ni 9.7 na miundombinu ya maji taka ni Sh milioni 143.2 na kwamba jumla ya fedha zilizookolewa katika miradi ni 493.

Hata hivyo Kamanda Suta aliwataka wakurugenzi wa halmashauri za wilaya kuwa watawachukulia hatua kwa kuwa fedha zimekuwa zikiliwa na wakusanyaji mapato wakati wao wakiwa maofisini badala ya kuwachukulia hatua wanasubiri Takukuru ishughulike.

Alisema sakata la Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje kutowalipa madiwani zaidi ya Sh milioni 40 za malimbikizo ya posho zao, limetokana na uzembe wake kwa kuwa ameshindwa kuwasimamia watendaji aliowapa dhamana ya kukusanya mapato.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,882FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles