24.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Taasisi ya Mtetezi wa Mama yapinga maandamano

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Taasisi ya Mtetezi wa Mama imepinga maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yaliyopangwa kufanyika Januari 24, mwaka huu yakiwa na lengo la kuishinikiza Serikali kuondoa miswada mitatu Bungeni.

Akizungumza na waandishi wa habari Januari 20,2024 jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Hamasa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwinyi Ludete amesema hoja walizozitoa CHADEMA hazina mantiki bali wanataka kuharibu taswira ya nchi.

“Watanzania wanahitaji huduma zote za kijamii zikiwemo maji,afya na elimu ambavyo vyote vimepatikana kupitia katiba hii iliyopo ambapo Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan anayatekeleza tena kwa vitendo,” amesema Ludete.

Ameongeza kuwa hoja ambazo wamezitoa CHADEMA ikiwemo ya katiba mpya ni hoja inayotaka majadiliano na ni mchakato unaozingatia vipaumbele ambapo kipaumbele cha serikali ni ridhaa ya wananchi katika kuleta maendeleo.

Naye Mwenyekiti wa Mtetezi wa wa mama Mkoa wa Dar es Salaam, Mohammed Chande amesema uhamasishaji wa maandamano unaofanywa na CHADEMA ni kuishiwa kwa hoja.

Amesema wao kama watetezi wamekitaka chama hicho kutoa hoja zao na kuziweka kwenye majadiliano lakini si kukimbilia barabani kwani huko kunaonyesha anguko lao.

“Sisi kama Taasisi ya Mtetezi wa Mama tunaiunga mkono Serikali na tumejipanga kumsemea Rais wetu kwa hoja za msingi na kama ilivyo kauli yetu ukimvaa Mama tunakuvaa kwa hoja,hivyo ni wakati wa wao kuleta hoja zao lakini si kusababisha fujo na kuiondoa amani ya nchi yetu,” amesema Chande.

Amesema kukosekana kwa hoja ya msingi kumewafanya kuja na hoja za kulazimisha na kuhamasisha maandamano.

Amesema siasa haihitaji hasira bali inahitaji mapinduzi ya mawazo na akili ili kujenga demokrasia ya kweli nchini.

Ametoa wito kwa wananchi kutojitokeza kwenye maandamano hayo badala yake viongozi wa CHADEMA wanapaswa kuchukua familia zao na kuanza kuandamana na si kutumia vijana.

“Nyinyi mnazo nchi za kukimbilia tunaomba mtuachie nchi yetu salama sisi tunataka amani maana Tanzania ndio mama yetu na ndio baba yetu hatuna nchi nyingine zaidi ya hii,”ameongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles