23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Sudan, ICC zachunguza mapendekezo kesi ya al Bashir

KHARTOUM, SUDAN

SERIKALI  ya Sudan imetangaza kuwa inajadiliana na Mahakama ya Kimataiifa ya Jinai (ICC) mapendekezo matatu kuhusu jinsi ya kumfungulia mashtaka rais wa zamani wa nchi hiyo, Omar al Bashir na wenzake kadhaa kwa tuhuma za kutenda jinai dhidi ya binadamu na jinai za kivita katika jimbo la Darfur.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Sheria wa Sudan, Nasruddin Abdul Bari, baada ya mazungumzo yake na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya ICC, Fatou Bensouda mjini Khartoum. 

Abdul Bari alisisitiza kuwa Sudan iko tayari kushirikiana na mahakama hiyo kwa mujibu wa sheria za kimataifa zinazoshughulikia wahalifu.

Aliongeza kuwa Sudan imetoa mapendekezo matatu kuhusu kesi ya al Bashir na wenzake ambayo ni ama kuanzishwa mahakama maalumu, kufunguliwa mahakama mseto inayoshirikisha serikali ya Khartoum na ICC, au kupelekwa watuhumiwa hao katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai huko The Hague nchini Uholanzi.

Al Bashir anakabiliwa na tuhuma za kutenda jinai dhidi ya binadamu huko Darfur

Waziri wa Sheria wa Sudan amesema kuwa pande hizo mbili bado zinajadili mapendekezo hayo.

Kwa upande wake Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC,  Fatou Bensouda alipongeza mazungumzo ya ujumbe wa mahakama hiyo na serikali ya Sudan bila ya kutoa maelezo zaidi.

Bensouda anajaribu kuwashawishi viongozi wa Sudan waafiki suala la kukabidhiwa al Bashir na maofisa wengine kadhaa wa zamani wa nchi hiyo ili wahukumiwe katika mahakama ya kimataifa ya ICC.

 ICC inamtuhumu al Bashir kwamba alihusika na mauaji ya kimbari dhidi ya wakazi wa eneo la Darfur huko magharibi mwa Sudan na vilevile kutenda jinai dhidi ya binadamu na imetoa kibali cha kutiwa nguvuni mtuhumiwa huyo.

AFP

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles