24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

SMZ yaridhishwa na miradi inayotekelezwa na TBA

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeridhishwa na miradi inayotekelezwa na  Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambapo kupitia Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) imeahidi kufanya miradi yenye kiwango kama hicho visiwani Zanzibar.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa Novemba 26, 2021 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Joseph Kilangi wakati akizungumza katika ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na TBA jijini Dodoma.

Katibu Mkuu huyo alikuwa ameongozana na wataalamu wa Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) ambapo walitembelea miradi ya Mji wa Kiserikali Mtumba awamu ya pili,ujenzi wa nyumba 3500 za watumishi wa umma,Nzuguni ambao umeanza na nyumba 150 na mradi wa ujenzi wa nyumba 20 za viongozi katika eneo  la Kisasa Jijini humo.

Katibu Mkuu huyo amesema kwa sasa wanaiamini TBA kwa asilimia mia moja hivyo watashirikiana na ZBA kutekeleza miradi mbalimbali visiwani Zanzibar kwa lengo la kupata miradi yenye ubora kama Tanzania Bara.

“Sasa mimi nadhani  tuiamini TBA kwa asilimia miamoja kama tunamiradi tutakayoianzisha basi TBA na wana miradi Zanzibar tutawaleta wataalamu wetu waje wafanye kazi kwa pamoja na TBA.

“Wanzanzibar wategemee tutawaalika TBA Zanzibar, wategemee mambo mazuri hizi fedha tulizopata tuna bilioni 460 zinaenda mifukoni mwa watu kupitia miradi mbalimbali.Tutawaiba waje Zazibar wasimamie miradi yetu,”amesema.

Aidha,Katibu Mkuu huyo amesema mradi wa Mji wa Serikali awamu ya pili ni mzuri na utaonesha kwamba Dodoma ni Makao Makuu ya Serikali kama ilivyo Lagos na ndoto ya Hayati mwalimu Julius  Kambarage Nyerere itakuwa imetimia kwa vitendo.

“Mradi ule wa Mji wa Serikali ni mzuri sana na majengo yale hasa awamu ya pili ikikamilika mji utakuwa ni mzuri sana lakini itaonesha kwamba hapa ni Makao Mkuu ya Nchi hata ukienda Lagos utaona hili nadhani ile ndoto ya Baba wa Taifa itatimia.

“TBA wamekuja na michoro mizuri na inajengwa kileo sana mazingira ni mazuri na vitendea kazi vimezingatia ubora,baada ya miaka miwili mitatu itaonekana kweli ni makao makuu ya Serikali,”amesema.

Kuhusiana na nyumba za watumishi wa umma zinazojengwa na TBA,Katibu Mkuu huyo amesema mradi huo utakuwa na manufaa makubwa kwani watumishi wataweza kukaa katika nyumba nzuri.

Hata hivyo,Katibu Mkuu huyo ameipongeza TBA kwa kufanya kazi nzuri ikiwa ni pamoja na kuwa na vifaa pamoja na wataalamu wa kutosha.

“Mimi kwa TBA kwakweli kwa uwezo nilioouna mimi nadhani hata kama kuna wakandarasi wengine kuna miradi mbalimbali ya ujenzi ni kushawishi tu waitumie TBA kama ni Mkandarasi waitumie TBA  kama ni msimamizi kwa sababu wana uwezo wote wana vifaa wana zana na wana wataalamu wa kutosha,”amesema.

Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) Eng Kassim Omar amesema lengo la ziara hiyo ni kujifunza yale ambayo TBA wanayafanya ambapo amedai kwa kiwango kikubwa yanalingana na majukumu ya ZBA.

Amesema kwa Zanzibar kwa sasa wapo katika matayarisho ya Mji wa Kiserikali visiwani humo ambapo amedai utekelezaji wao utakuwa ni mkubwa ambapo amewakaribisha TBA waone yale ambayo wameyaonesha tutakavyoyatekeleza.

Naye,Kaimu Mkurugenzi Idara ya Miliki TBA,Said Mndeme amesema ziara hiyo imekuwa na manufaa makubwa kwani ZBA  wameweza kuona mradi wa nyumba za watumishi wa umma na wameona jinsi walivyoutekeleza mradi huo na   wameweza kujionea jinsi ambavyo  wamejipanga katika eneo la  material pamoja na viwanda mbalimbali ambavyo wamevianzisha.

Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya ujenzi TBA,Likimaitare Naunga ameishukuru ZBA kwa kuichagua TBA kama sehemu ya kupata uzoefu katika sekta ya ujenzi ambapo amedai wapo tayari kwa ajili ya ushirikiano huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles