Sita wauawa kwa risasi Mtwara

0
1081
Wanakijiji wa Ngongo Wilaya ya Tandahimba, wakismsikiliza Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz.

Florence Sanawa, Mtwara

Watu sita raia wa Tanzania wameuawa kwa kupigwa risasi na wengine saba kujeruhiwa wakiwa katika kisiwa cha Mto Ruvuma mkoani hapa na watu wanaodaiwa kuwa wahalifu kutoka nchi jirani ya Msumbiji.

Akizungumza baada ya kutembelea Kijiji cha Ngongo Wilaya ya Tandahimba Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana katika eneo hilo ambalo hufanya shughuli zao za kilimo.

“Vyombo vya ulinzi na usalama vitahakikisha wahalifu hao wanapatikana na sheria kali zitachukuliwa juu yao, niwasihi tu wananchi kuepuka kwenda nchi za watu bila kuwa na vibali,” amesema.

Kwa upande wake Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa jeshi hilo, Leberatus Sabas, amesema serikali haitakubali mambo ya hovyo hovyo kam ahayo kutokea ambapo amesisistiza kuwa damu ya Mtanzania haiwezi kupotea bure kwani aliyeua kwa upanga nae atauawa kwa upanga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here