25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 1, 2024

Contact us: [email protected]

SIMU YA ZITTO YAZUIWA POLISI KWA UCHUNGUZI

PATRICIA KIMELEMETA NaCHRISTINA GAULUHANGA-DAR ES SALAAM


SIMU ya Kiongozi Mkuu wa Chama Cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, imechukuliwa na polisi kwa ajili ya uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkali.

Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, anadaiwa  kutoa taarifa za takwimu za uongo na kuzisambaza katika mitandao ya jamiii.

Zitto alikuwa akizungumza na waandishi wa habari  Dar es Salaam jana baada ya kumaliza mahojiano kwenye Kituo cha Polisi cha Kamata katika kitengo kinashughulika na uhalifu wa fedha na mtandao.

Alisema polisi waliamua kuchukua simu hiyo   kuangalia mawasiliano yake ikiwamo kudaiwa  kusambaza takwimu za uongo kwenye mitandao ya  jamii ikiwamo Twitter.

Alisema kwa sababu kitengo hicho kinashughulika na makosa ya mtandao (Cyber Crime), wanapaswa kuchukua simu hiyo  waweze kujiridhisha na wanachodhani.

“Nitakua nje ya mawasiliano kwa muda kidogo mpaka polisi watakaponirudishia simu yangu kwa sababu ni haki yao kuchukua mawasiliano yangu na kuyafanyia uchunguzi   wanapoona kuna shaka,” alisema Zitto.

Alisema  kwa sababu kosa wanalomtuhumu la kudai kuwa alitoa takwimu za uongo na kuzisambaa limejikita kwenye mitandao ya  jamii, hali inayowaruhusu kutekeleza majukumu yao.

Zitto alisema kwa sababu hiyo,  watu watakaomtafuta kwa kipindi hicho wanapaswa kujua kuwa hana mawasiliano yoyote ya simu mpaka polisi watakapomaliza kazi zao na kumrudishia.

Akizungumzia kuhusu kutenguliwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bukoba Erasto Mfugale na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Vijijini, Mwantumu Dau, alisema ni udhalilishaji.

“Rais anaweza kuwakatisha tamaa watendaji wake kutokana na kitendo chake cha kuwaita hadharani na kuwatumbua hata kama ana mamlaka ya sheria,” alisema.

Zitto ametakiwa kurudi kituoni hapo Novemba 21.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles