22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

WAFUGAJI WAASWA KUFUGA KISASA

Na ANNA RUHASHA



MKUU wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole, amewataka wafugaji kufuga kisasa kuondokana na migogoro inayotokana na kundi kubwa na ng’ombe na kukosa sehemu za malisho.

Kipole alitoa kauli hiyo juzi wakati wa uzinduzi wa kupiga chapa wa mifugo lililoanzia katika Kata ya Kishinda.
Alisema migogoro mingi baina ya serikali na wafugaji inatokana na kundi hilo kukosa sehemu ya malisho.

“Fugeni kisasa unaweza ukafuga ng’ombe mmoja ukazalisha lita tano za maziwa sawa na mfugaji wa zamani ambaye ana ng’ombe 10 lakini anapata lita mbili za maziwa.

“Hii itasaidia kupunguza migogoro ingawa wilaya yangu haijawahi kutokea migogoro hiyo,”alisema Kipole.
Alisema hatua hiyo ya kupiga chapa nifugo itawasaidia katika utambuzi na kupunguza wizi na mwingiliano wa ng’ombe kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyigine na halitakuwa na madhara yoyote wakati wa kupeleka mifugo hiyo minadani.

“Chapa hii itasaidia sana faida yake ni utambuzi, kupunguza wizi na uvamizi wa mifugo mingine kutoka maeneo tofauti.
“Niwasihi chapa hii siyo ombi ni lazima na atakayekaidi faini yake ni Sh milioni mbili kila kundi, lakini niwapongeze kwa sababu mmejitokeza kwa wingi,’’ alisema.

Kipole alisema Serikali inategemea mchango mkubwa kutoka kwa wafugaji kuhusu sera ya viwanda.
Aliwasihi wafuge sana kusaidia viwanda vya kuchakata ngozi na maziwa viweze kuzalisha kwa wingi na kuongeza ajira kwa vijana .

Mtaalamu wa ngozi na Mkaguzi wa Nyama wa Wilaya, Morisi Ndiyo, alisema chapa hiyo haina madhara sana katika kushusha thamani ya ngozi.
Mmoja wa watekelezaji wa hatua hiyo, Gabriel Komanya aliiomba serikali kuboresha mazizi wanayofanyia shughuli hizo , vitendea kazi kama viatu na kuboresha mihuri kutokana na kutoshika vizuri wakati wa uchapaji huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles