23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Simba yatuma salamu Azam

 WINFRIDA MTOI, DAR ES SALAAM 

KIKOSI cha Simba kimetua jana, jijini Dar es Salaam na kwenda moja kwa moja kambini kuindalia mauaji Azam FC wanayokutana nayo kesho. 

Wanamsimbazi hao ambao tayari wameshatangazwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, msimu wa 2019/2020, wataikabili Azam katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam 

Simba imechukua ubingwa baada ya kufikisha pointi 79, ilizopata kutokana na michezo 32, ikiwa ni taji la tatu mfululizo. 

Akizungumza baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, alisema hakuna kulala mpaka kieleweke. 

Alisema wachezaji wake wako fiti na leo wanatarajia kuendelea na mazoezi ya kujiandaa na mechi hiyo, lengo ni kuhakikisha wanafika fainali na kuchukua kombe hilo. 

Sven alisema awali ilikuwa ni kupigania kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu, wamefanikiwa, hivyo wachezaji wana morali ya kuhakikisha wanaendeleza makali FA. 

“Katika mechi mbili tulizokwenda kucheza Mbeya, lengo letu lilikuwa ni kupata pointi hata moja na tumefanikiwa kwa sasa nguvu tunaelekeza FA na huko naamini tutafanikiwa,” alisema. 

Naye nahodha wa timu hiyo, John Bocco, alisema wameshasahau kilichotokea 

 Mbeya, hivyo wanaweka ubingwa pembeni na kufanya kazi ya kupigani kombe lingine la mchuano ya ASFC.

Alisema wachezaji wote wako vizuri na wamefurahi kutimiza malengo ya klabu ya kutetea ubingwa, kilichobaki ni kuendelea kuwapa furaha Wanasimba katika mechi zilizobaki.

“Tumechukua ubingwa si kwamba tumemaliza kazi, huu tunauweka mbeni kwa sasa na nguvu tunaelekeza kombe la shirikisho tukianza na Azam keshokutwa (kesho),” alisema Bocco.

Alieleza kuwa mchezo wao na Azam siku zote unakuwa ni mgumu, huo umekuwa kama utamaduni kutokana na wachezaji wa timu hiyo kufahamiana vizuri.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Haji Manara, alisema mchezo huo wanataka kushinda na baada ya hapo wanatangaza sherehe za ubungwa.

“Tumeshawaambia mashabiki wetu waje uwanjani kwa wingi, kwa sababu tumekubaliana wote kusitisha sherehe za ubingwa hadi tutakapomalizana na Azam,” alisema Manara.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,460FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles