24.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 30, 2023

Contact us: [email protected]

Simba kuingia kivingine uwanjani kesho

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Kocha Msaidizi wa Simba, Suleiman Matola, amesema huenda kukawa na mabadiliko ya kiufundi katika mchezo wa kesho dhidi ya Yanga utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Matola amesema mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na aina ya timu wanayokutana nayo lakini lazima washinde kwasababu wanahitaji ubingwa.

“Nia yetu ni ni kutetea vikombe vyetu vyote, tunajua siku zote mechi ya derby sio rahisi na sisi kwa kutambua ugumu wake tumejiandaa kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi.

“Kiufundi tumekuwa tukibadilika kutokana na aina ya timu tunayocheza nayo, hata kesho tutegemee mabadiliko. Wachezaji tutakaowakosa ni Ibrahim Ajib ambaye anaumwa malaria na Jonas Mkude kila mtu anajua matatizo yake,” amesema Matola.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,198FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles