31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

SIMBA HAKUNA KULALA

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KIKOSI cha Simba kinatarajia kuendelea na mazoezi kesho ikiwa ni mipango ya kujiweka fiti kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara, zinazowakabili mbele yao.

Wachezaji hao walipewa mapumziko ya siku tatu baada ya kumaliza mchezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons, ambao ulimalizika kwa suluhu katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kwa sasa Simba inakabiliwa na mchezo wa Ligi dhidi ya Ruvu Shooting, unaotarajiwa kuchezwa Novemba 24 mwaka huu katika dimba hilo la Uhuru.

Kikosi hicho kitaanza mazoezi huku wakiwakosa baadhi ya wachezaji walioenda Timu ya Taifa akiwemo Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Gadiel Michael, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Miraji Athuman na Hassan Dilunga.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kocha wa viungo wa timu hiyo, Adel Zrane, alisema baada ya kufanya mazoezi ya mwisho siku ya Ijumaa asubuhi waliwapa mapumziko ya siku tatu.

“Jumanne ndio tutaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiweka fiti baada ya ligi kusimama kwa muda kupisha maandalizi ya Timu ya Taifa ambapo kuna baadhi ya wachezaji wameenda huko,” alisema.

Alisema baada ya kuanza mazoezi ndio watafahamu programu yao katika kipindi hiki baada ya Ligi kusimama kwa muda.

Simba inashika usukani katika msimamo wa ligi wakijikusanyia pointi 22 baada ya kushuka dimbani mara tisa na kushinda michezo saba huku wakitoa sare moja na kupoteza mmoja.

- Advertisement -
Previous articleTAIFA STARS YANOGA
Next articleWarejeshwa

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,625FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles