27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Shambulio la Al Shabab Kenya laua mmoja, 10 wajeruhiwa

Anna Potinus


Mtu mmoja anadaiwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 10 kujeruhiwa katika shambulio la kigaidi linalodaiwa kufanywa na kundi la kigaidi la Al Shabab jijini Nairobi, nchini Kenya.


Shambulio hilo limetokea leo jioni katika Hoteli ya kifahari ya Dusit iliyopo eneo la Riverside Drive na majeruhi hao walikimbizwa katika hopitali mbalimbali mjini hapo ikiwamo Hospitali Kuu ya Kenyatta, Aga Khan na Hospitali ya Avenue.


Kwa mujibu wa Kituo cha Television cha Citizen cha nchini humo, majeruhi hao wanaendelea na matibabu katika hospitali hizo huku wananchi wakiombwa kufika na kuchangia damu kwa ajili ya wagonjwa hao.


“Baadhi ya hospitali zimeita wanaotaka kutoa damu kwa lengo la kuwasaidia waliojeruhiwa katika mlipuko huo lakini pia maofisa wa polisi wako katika maeneo ya hospitali walizopelekwa majeruhi wa ajili ya kufanya doria,” imesema taarifa ya Citizen.


Naye Inspekta Jenerali wa Polisi, Joseph Boinet, amewataka wananchi kuwa watulivu na kufuata maelekezo wanayopewa na askari wakati zoezi la uokoaji likiendelea na uchunguzi ukiendelea kufanywa.


“Operesheni inaendelea na sisi tunawaombea wale walioathirika waweze kupata nafuu mapema pia tuko katika hali kufanya uchunguzi tukio hilo limeathiri kwa kiasi gani pia tunawaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa maofisa wa polisi na kufuata maagizo watakayokuwa wanapewa,” amesema.


Inadaiwa washambuliaji hao walifika na magari mawili madogo na moja liliegeshwa kando ya magari mengine mawili ambapo lililipuka majira ya saa 11 alasiri na muda mfupi baadaye maofisa wa usalama walianza kufanya zoezi la uokoaji na mshambuliaji mmoja aliingia na miguu katika eneo hilo na kujilipua.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,549FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles