28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Sh bilioni 228 kumalizia maboma ya madarasa, zahanati

RAMADHAN HASSAN-DODOMA

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, amesema kwa mwaka wa fedha 2020/21 Serikali imetenga Sh bilioni 228 kwa ujenzi wa maboma ya madarasa na zahanati ambapo alidai kwamba ana uhakika Serikali itatoa fedha.

Kauli hiyo aliitoa jana bungeni wakati akijibu hoja za wabunge waliohoji kuhusu umaliziwaji wa maboma ya zahanati, ujenzi wa shule na vituo vya afya.

“Mheshimiwa Naibu Spika tumetenga Sh  bilioni 228 kwa mwaka wa fedha 2020-2021 na hizo tunaenda kuzitoa,” alisema Dk. Kijaji.

Alisema Serikali imetoa Sh bilioni 19.5 katika bajeti ya mwaka 2019/20 kukamilisha ujenzi wa nyumba za walimu 364 na zahanati 52.

Dk. Kijaji alisema Serikali ilitenga Sh bilioni 19.5 katika mwaka wa fedha 2019/20 kwa ujenzi wa nyumba 364 za walimu pamoja na zahanati 52.

Alisema kwamba fedha hizo Serikali imeishazitoa  zote.

 Dk. Kijaji alisema  kwa mwaka wa fedha 2017-2018 Serikali ilitenga jumla ya Sh bilioni 38 kwa ujenzi vituo vya afya 96 ambapo alidai kwamba fedha hizo zote zilitolewa.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles