31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Serikali yawakumbusha vijana kuwa waaminifu mikopo ya vikundi

*Ni Bilioni 1 inayotengwa na Serikali kila mwaka

*Yasema wengi wanapopata mikopo hubadili malengo

Na Fraja Masinde,Mtanzania Digital

Serikali imewahimiza vijana kuhakikisha kuwa wanatumia vyema mikopo wanayopewa ili waweze kujikwamua kiuchumi na kusaidia wengine.

Wito huo umetolewa Dar es Salaam leo Agosti 10, 2022 na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu, Patrobas Katambi hafla ya hoja za maongezi kuelekea Siku ya Kimataifa ya Vijana Agosti 12.

Katambi amesema kuwa pamoja na Serikali kupitia ofisi ya Waziri Mkuu kutenga Sh bilioni 1 kila mwaka kwa ajili ya kusaidia vijana lakini baadhi yao wamekuwa siyo waaminifu pindi wanapokopeshwa fedha hizo.

“Tunashukuru kwasasa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kila mwaka inatenga fedha Sh bilioni 1 kwa ajili ya mikopo yenye masharti nafuu kwa vijana ambapo takribani viku 586 vimenufaika kwenye Halmashauri za wilaya 155.

“Changamoto ni vijana kutokuwa waaminifu pindi wanapokopeshwa fedha hizi, kwani wakishachukua mkopo malengo yanabadilika na kufanya mambo mengine ambayo hayakukusudiwa awali.

“Hii imefikia hatua vikundi vingi baada ya kuchukua fedha vinabadilisha malengo na hatimaye kusambaratika, hivyo inakuwa changamoto kwa fedha kurejeshwa, lakini pamoja na hayo vipo vikundi ambavyo vinafanyavizuri na vinajitahidi kurejesha fedha.

“Mfano Dar es Salaam ni moja ya Mikoa inayofanya vizuri ndiyo maana hata mikopo imekuwa ikiongezeka,” amesema Katambi.

Katambi amesema kuwa kwa mkoa wa Dar es Salaam zaidi ya Sh bilioni 50 zimetolewa kwa vijana huku Sh bilioni 10 pekee ndizo zilizorejeshwa.

“Hata hivyo tutachukua ushauri wa Naibu Mwakilishi wa UNFPA, Dk. Wilfred Ochan ambaye anasema ni bora asilimia 50 ya mkopo ikatumika kutoa vifaa vya shughuli inayoombewa mkopo, kwani tunajua hata akikimbia hawezi kukimbia na trekta badala yake litasaidia watu wengine wenye uhitaji,” amesema Katambi.

Aidha, katikahatua nyingine Katambi amesema kuwa baadhi ya watendaji wa serikali nao wamekuwa ni changamoto kwenye utoaji wa mikopo hiyo.

“Changamoto nyingine ni watendaji wa serikali ambao wamekuwa sio waaminifu kwani mkopo unaombwa Sh milioni 10 lakini vijana wanapewa milioni 7, hili ni jambo pia linalokwamisha mpango huu.

“Kwani lengo la serikali ni kuona maisha ya vijana yakibadilika, kutoka hatua moja kwenda nyingine, hivyo tunaendelea kuwahimiza vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa kwani yeyote ambaye anautayari wa kufanya vizuri serikali ipo tayari kumsaidia ikiwamo kumpa elimu,” amesema Katambi.

Akizungumzia asasi za kiraia amesema kuwa nazo zimekuwa ni changamoto wakati mwingine kutokana na kile wanachokitoa kwa vijana.

“Changamoto ni asasi za kiraia wapo tunaowatambua na wengine hatuwatambui, mfano vijana wanafundishwa uzalendo tunajua wanaambiwa nini huko, sera za nchi, mipango na mikakati ya serikali wanaifahamu? Lazima tupime tija inayotolewa na asasi hizi,” amesema Katambi.

Pia amesisitiza kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na UNFPA katika kuhakikisha kuwa inasaidia vijana kufanikisha malengo yao huku akiwahimiza kujitokeza Agosti 23, kwa ajili ya kushiriki Sensa.

Kila mmoja anahusika katika kujenga uchumi imara, ustawi na maendeleo endelevu, Jiandae kuhesabiwa hivyo inaendana na mipango ya Tanzania ambapo tunasensa Agosti 23, mwaka huu itakayowezesha kuweka mipango thabiti ya vijana.

Hatua hiyo itawezesha serikali kuwakumbuka vijana kwenye nyanja mbalimbali ikiwamo elimu, biahara na mambo mengine, kwani takwimu hizo zitasaidia katika uandaaji wa bajeti.

“Vijana ndio chachu ya maendeleo katika taifa lolote, wenye kuleta mapinduzi,ndiyo maana takwimu zinaonyesha kuwa katika idadi ya watu wote duniani ambayo ni bilioni 8 kati yao vijana ni bilioni 1.8.

Aidha, kwa hapa nchini utafiti unaonyesha kuwa vijana chini ya miaka 35 ni milioni 18.3 huku wenye uwezo wa kufanyakazi wakiwa ni milioni 14.6 sawa na asilimia 80.

Upande wake Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi(UNFPA), Dk. Wilfred Ochan amesema ushiriki wa vijana ni muhimu katika kusukuma maendeleo ya taifa ndiyo sababu wanashirikiana na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kuwa vijana wanazifikia fursa zilizopo.

Dk. Ochan amesema kuwa UNFPA itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha kuwa vijana wanakuwa ni sehemu ya maendeleo ya taifa na kutoa mchango wao kikamilifu.
“UNFPA imejitolea kusaidia vijana na mashirika ya vijana, ahadi hii imetekelezwa katika dhamira yetu, mpango mkakati, mkakati wa vijana na mpango wa utekelezaji wa mkutano wa kimataifa wa idado ya watu na maendeleo(ICPD).

“Ulimwenguni kte vijana husema hakuna chochote chetu bila sisi, UNFPA tumesiakia, tumejifunza na kutilia maanani kauli hii, ushirikiano wetu na vijana ni lazima kila wakati uwe kulingana na ushiriki wao wa dhati,” amesema Dk. Ochan.

Aidha, Dk. Ochan amesema kuwa kwa mwaka 2021 UNFPA na washirika kupitia mpango wa elimu rika walifikia zaidi ya vijana 125,000 wenye taarifa sa afya na haki za ujinsia na uzazi.

“Niwahimize pia vijana kujitokeza Agosti 23 kwa ajili ya sensa kwani data ni muhimu ili kufahamisha ufanyaji wa maamuzi kuhusu ugawaji wa wa rasilimali na sera, ikiwa ni pamoja na zile zinazowalenga vijana,” amesema Dk. Ochan.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles