23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Serikali yaunda tume kuchunguza ajali ya moto TANESCO Morogoro

Na Ashura Kazinja, Morogoro.

SERIKALI ya Mkoa ya Morogoro imeunda Tume maalumu ya kuchunguza tukio la ajali ya moto lilitokea katika kituo cha kupokea, kupoza na kusambaza umeme cha Shirika la ugavi la umeme Tanzania (TANSECO) kilichopo eneo la Msamvu.

Kituo hicho kinachopokea umeme kutoka Bwawa la kufua umeme la kidatu kinahudumia mikoa ya Morogoro , Dar es Salaam na ile ya kaskazini.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela amesema chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika na itaundwa tume kuchunguza tukio hilo.

Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Inspekta Neema Msokwa, amesema moto huo umenza mnamo majira ya saa mbili asubuhi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro (SACP) Fortunatus Musilimu amesema hakuna madhara yoyote kwa binadamu yaliyotokea mbali na kuungua vifaa ikiwemo transfoma zinazopoza na kusambaza umeme.

Kwa upande wake Meneja wa TANESCO Mkoa wa Morogoro Mhandisi Fedgrace Shuma amesema kituo hicho kimeungua kwa asilimia kubwa na kwamba jitihada za haraka za kurejesha huduma ya umeme kutoka Chalinze na Mkoa wa Dodoma zinaendelea kufanyika.

Hata hivyo Maeneo yaliyoathirika kwa kukosa huduma ya umeme ni Manispaa ya Morogoro, Wilaya ya Mvomero, Kilosa, Mvuha pamoja na maeneo meingine yanayotumia laini inayotoka Msamvu kituo cha kupoozea umeme, ikiwemo mikoa ya jirani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,301FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles