21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, August 16, 2022

Serikali yatoa Sh bilioni 688 kwa wanaojenga Stiglier’s George

LEONARD MANG’OHA -DAR ES SALAAM

SERIKALI imeikabidhi kampuni ya Arab Contractors hundi Sh bilioni 688.645 kama malipo ya awali ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bwawa la umeme katika maporomoko ya bonde la Mto Rufiji (Stiglier’s George) unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Akikabidhi hundi hiyo Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James, alisema kiasi hicho cha fedha ni   asilimia 70 ya malipo ya awali ya mradi huo.

Alisema kwa mujibu wa mkataba   na kampuni hiyo, Serikali ilitakiwa kutoa Sh trilioni moja kama malipo ya mradi huo ambayo ni   asilimia 15 ya fedha zote zinazopaswa kulipwa kwenye mradi huo.

Alisema asilimia 70 ya kiasi hicho cha fedha kilipaswa kulipwa kwa Dola za Marekani ambazo ni milioni 309.645 na asilimia 30 ya zitalipwa kwa shilingi.

“Desemba  12, 2018 Serikali ilisaini mkataba na mkandarasi kampuni ya Arab Contractors “Osman A. Osman & Co” and Elsewedy Electric S.A.E (JV AC – EE) wenye thamani ya Sh trilioni 6.558 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa maji wa mto Rufiji wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 2,115,” alisema.

Doto alisema kukamilika kwa mradi wa huo wa Mto Rufiji kutakuwa ni kichocheo katika kuwezesha Tanzania kufikia azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

 Alisema mradi huo utasaidia kupatikana   umeme wa uhakika utakaosaidia maendeleo ya uchumi wa viwanda na maendeleo endelevu ya wananchi kwa ujumla.

Alizitaja faida nyingine kuwa ni uwekezaji katika sekta ya viwanda, sekta mbalimbali za uchumi na kuongezeka kwa uzalishaji viwandani, kuongezeka kwa ajira takribani 4,500 hadi 6,000 wakati wa ujenzi na ajira 100 za wataalamu wa kusimamia kituo baada ya ujenzi.

 “Ni matumaini yangu kuwa mkandarasi atafanya kazi usiku na mchana  kukamilisha ujenzi wa mradi huu muhimu ndani ya kipindi cha miezi 36 kama ilivyo katika mkataba,” alisema Dotto.

  Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dk. Hamisi Mwinyimvua, alisema Aprili 15, benki za CRDB na UBA zilitoa dhamana za malipo ya awali na utendaji kazi kwa mkandarasi kwa mujibu wa mkataba wa ujenzi wa mradi huo uliosainiwa Desemba mwaka jana.

“Kutolewa kwa dhamana hizo kuliwezesha kuanza kwa hatua za utekelezaji wa mradi ikiwa ni pamoja na Serikali kumlipa mkandarasi malipo ya awali hatua inayofanyika hivi leo.

 “Kiasi kilicholipwa leo hii ni asilimia 70 fedha za kigeni Dola za Marekani 309 645,188.07  (Sh 688,650,267.57) Sehemu ya fedha za hapa asilimia 30 zitalipwa mara baada ya mkandarasi kukamilisha taratibu za  mkataba zinazohusu malipo hayo.

“Ninao uhakika kuwa malipo ya awali yaliyofanyika leo yatamwezesha mkandarasi sasa kukamilisha taratibu za kupeleka vifaa katika eneo la mradi mara moja kwa mujibu wa mkataba,” alisema Dk. Mwinyimvua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,814FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles