26.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Serikali ya wanyonge mnatusikia wanyonge?

na EMMANUEL MWANSASU

WANYONGE wanyonge wanyonge, neno wanyonge linasikika sana miaka ya karibuni haswa tangu awamu hiii ingie madarakani na Serikali yetu imekuwa ikijinasibu mara nyingi kuwa hii ni Serikali ya wanyonge lakini bado nina mashaka kama kweli Serikali hii ya wanyonge inatusikiliza wanyonge.

Ukitaja wanyonge kwenye nchi hii basi unataja namba kubwa ya watu ambayo inaweza kuchukua zaidi yaasilimia sitini na kama hukubaliani na hili hebu fanya utafiti mdogo kwenyesehemu zinazotoa huduma za kijamii, ukiangalia kwa sehemu kubwa utaona wananchi wengi wa hali ya chini hukimbilia kwenye vituo vya umma leo hii ukienda Kairuki Hospitali huduma inayotolewa pale si sawa na huduma inayotolewa Mwananyamala Hospitali,namba ya watu utakayoikuta katika hospitali hizo mbili ni tofauti kabisa hapo hujatembelea shule za Kayumba almaarufu shule za Kata ulinganishe na shule kamaAl Muntazir na nyinginezo, hivyo mara nyingi ninapokuwa nasikia serikali ya wanyonge itatupigania wanyonge imani yangu ya kwanza huwa ni  inayopunguziwa gharama na ukali wa maisha lakini kwa bahati mbaya siyaoni hayo yakitokea na hiyo ndio sababu inayonifanya nijiulize Je, Serikali ya wanyonge hivi inatusikia kweli wanyonge?

Leo nitatumia maeneo matatukujaribu kuonesha ni kwa namna gani bado wanyonge hatukwamuliwi kwenye changamoto tulizonazo, maeneo matatu nitayakozungumzia ni vibarua,wafanyabiashara na wananchi walioajiriwa.

Vibarua:  kwa kifupi kibarua ni mtu anayefanya kazi bila kuwa na mkataba, kufanya kwake kazi kunategemea huruma ya mwenye ajira ili yeye kuendelea kufanya kazi. Hili ni kundi ambalo linaweza kuwa linachukua namba kubwa ya wananchi wa Tanzania, kundi hili linabeba vijana wa bodaboda, kundi hili linajumuisha makondakta, vijana wanaofanya kazi viwandani, madereva wasio na mikataba. Nimeshasikia mara nyingi watu wa kwenye kundi hili wakililia waajiri wao kuwapa mikataba na wakati mwingine hufikia kuanzisha migomo lakini kwa bahati mbaya kwa sababu hawana mikataba matajiri  hawahangaiki nao kwa sababu wanafahamu fika kuwa bado watapata vibarua wengine wa kuwafanyia kazi.

Nimeona watu wakigoma kwenye viwanda, nimeona madereva wakigoma kudai mikataba lakini kwa bahatimbaya sijawahi kuona jitihada za kutosha za serikali kuhimiza kuwapigania wananchi wao, watu hawa tumeshindwa kuwa ajiri kwenye taasisi za kiserikali tumewaachia sekta binafsi lakini hata huko tunashindwa kuwapigania maslahi yaohivi kweli tunawasikiliza wanyonge? Mpaka leo kuna viwanda vinawalipa vibarua Sh.5000 kwa siku hivi hawa watu wanaishije? Mtuambaye hana mkataba bado analipwa Sh. 5000 mtu kama huyu anaachaje kuwa mwizi?Mnyonge huyu anakumbukwaje? Serikali ya wanyonge tunawakumbuka hawa?

Wafanyabiashara: Siku za karibuni nilijaribu kufanya utafiti mdogo kuona changamoto wanazokutana nazo wafanyabiashara hasa wale wa Kariakoo na nilichogundua ni kuwa wafanyabiashara wengi wanaumizwa na malipo ya Serikali, mfanyabiashara mmoja unaweza kumkuta analipa malipo ya makadirio, malipo ya leseni ya biashara, malipo ya kodi ya huduma (Service Levy), SDL, kuandaa hesabu ya mwaka na malipo mengine mengi na hawa ndio wananchi wanyonge wanaojitahidi kujikwamua kutoka kwenye umaskini sasa tnawasaidiaje hawa kuinuka, hapo sijazungumzia malipo ya ushuru wa usafi na malipo mengine, kwa kifupi hawa wanyonge wanaumia sana, hapa sijawazungumzia wafanyabishara wale wadogo wadogo ambao nimewahi kuandika malalamiko yao mara kadhaa, kwa kifupi wanyonge wanalia sana, wanaumia sana na wala hawaioni dira ya Serikali ya wanyonge kuwasikia basi Serikali ya wanyonge tuwasikie hawa.

Waajiriwa:kwasiku za karibuni hapa ndio pamekuwa na fukuto, nimeyaona malalamiko yawafanyakazi wakitoa malalamiko ya wao kupewa asilimia ishirini na tano tu kamakiinua mgongo na asilimia zinazobaki watalipwa ndani ya miaka kumi na miwili naendapo mstaafu atafariki katikati ya pensheni yake basi wanufaika watapokea mafao hayo kwa muda wa miaka mitatu tu sasa naomba tujiulize mambo hapa hawa wanyonge tunawainua ama kuwaangusha? Ukizungumza sekta ya ajira kuna wadau nakatika hao wadau waajiriwa nao ni sehemu ya wadau sasa kama wao wanalalamikakuhusu hili  haya maamuzi yalifanywa kwamaslahi ya nani?

Hawa wadau ambao ndiowananchi wanyonge au yalifanywa kwa faida za wengine? Serikali ya wanyonge kabla ya kufanya maamuzi haya tuliyafikiria haya? Mtu afanye kazi mpaka uzee wake wa miaka 55 mpaka 60 halafu bado tumpe pesa kidogo kidogo kama mtu aliyeomba hisani, hili ni jasho la mtu kwa nini tusiwaache wastaafu ama wafanyakazi waamue juu ya maslahi yao? Tukumbuke hizi pesa wastaafu wengi huzitegemea kufanya uwekezaji ambao utawafanya waendeshe maisha yao kwa amani. Imani yangu inaniambia serikali yetu ni serikali sikivu na kama kweli ni serikali sikivu naya wanyonge basi imani yangu ni kuwa tutawakumbuka ndugu zetu wastaafu kwenyehili.

Kama ukiwa kibarua ni shida, ukiwa mfanyabiashara na ukaamua kujiajiri ni shida na hata ukiajiriwa na kupewa mkataba nako shida sasa sisi wanyonge tunauliza Je, Serikali yetu wanyonge inatusikia? Na kama inatusikia mbona hatuoni ikitutafutia ufumbuzi waunyonge wetu?

Nawasilisha.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,451FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles