23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 9, 2023

Contact us: [email protected]

SERIKALI KUWATAMBUA WATOTO WENYE ULEMAVU

SERIKALI imesema kwa sasa zoezi la kuwatambua watoto wenye ulemavu linaendelea na kutoa wito kwa jamii kuwapatia fursa watoto hao sawa na watoto wengine.

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu, Stella Ikupa, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Fatuma Tawfiq (CCM).

Katika swali lake, Mbunge huyo alitaka kujua Serikali inatoa tamko gani kuhusiana na baadhi ya wazazi na walezi wanaowaficha watoto wenye ulemavu.

Aidha, alitaka kujua kauli ya Serikali kwa baadhi ya wazazi na walezi wanaowaficha watoto wenye ulemavu.

Akijibu swali hilo, Ikupa alisema Serikali inawatambua watu wenye ulemavu na wamekuwa wakitoa elimu kwa jamii kuhusiana na kutowaficha watoto wenye ulemavu.

Aidha, alisema kwa sasa zoezi la kuwatambua watoto wenye ulemavu linaendelea nchini kote.

Akitoa majibu ya nyongeza ya swali hilo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, aliwahakikishia wabunge kuwa Wizara yake imekuwa bega kwa bega na watoto wenye ulemavu na itaendelea kutoa vifaa kwa watoto wenye mahitaji maalumu.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalum, Khadija Nassir Ali (CCM), alitaka kujua Serikali inajua idadi kamili ya watu wenye ulemavu na aina ya ulemavu waliokuwa nao.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Ikupa alisema Tanzania inakadiriwa kuwa na takribani watu wenye ulemavu wapatao milioni 2.6 ambayo ni sawa na asilimia 5.8 ya Watanzania.

Alisema watu wenye ualbino 16,477 sawa na asilimia 0.04, kuona 848,530 sawa na asilimia 1.19, kusikia 425,322 sawa na asilimia 0.97, kutembea 525,019 sawa na asilimia 1.19, kukumbuka 410,931 sawa na asilimia 0.910, kujihudumia 324,725 sawa na asilimia 0.74 na ulemavu
mwingine 99,798 sawa na asilimia 0.23.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,351FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles