30.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 10, 2024

Contact us: [email protected]

Ruzuku kutoka REA yawezesha utekelezaji mradi wa umeme Kilolo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umesema utahakikisha unashirikiana na sekta binafsi katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora na nishati ya uhakika vijijini.

Mkurugenzi waTeknolojia za Nishati Jadidifu na Nishati Mbadala wa REA, Mhandisi Advera Mwijage alisema hayo baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa umeme wa maji (kilovoti 2400) wa Idete wilayani Kilolo unaotekelezwa na Kampuni ya Lung’ali Natural Resources Co ltd.

Amesema REA mpaka sasa imeishatoa ruzuku ya Sh bilioni 4 kwa mradi huo ulio chini ya Kanisa Katoliki mkoani Iringa ambazo zimetumika kwa utafiti wa mazingira, ujenzi wa bomba la maji na jengo lenye mtambo wa kuzalishia umeme (Power House).

Amesema REA mpaka sasa imeishatoa ruzuku ya Sh bilioni 4 kwa mradi huo ulio chini ya Kanisa Katoliki mkoani Iringa ambazo zimetumika kwa utafiti wa mazingira, ujenzi wa bomba la maji na jengo lenye mtambo wa kuzalishia umeme (Power House).

Pia, amesema REA ina wajibu wa kuwaunganisha wazalishaji wadogo na taasisi zinazotoa mikopo kwa riba nafuu ambapo Benki ya TIB imeikopesha kampuni hiyo ili ikamilishe mradi huo wa umeme kwa wakati na kuingiza kwenye gridi ya taifa.

“REA inafanya kazi na sekta binafsi katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora ya nishati vijijini na kuchangia katika shughuli za uchumi zinazoongeza kipato kwa wananchi,” alisema Mhandisi Mwijage.

Aliongeza kuwa serikali peke yake haiwezi kufanya kila kitu hasa katika miradi ya maendeleo inayogusa wananchi na hivyo kutambua umuhimu wa ushiriki wa sekta binafsi.

Serikali imekuwa ikiipatia REA fedha ili kuwawezesha kufadhili miradi ya wazalishaji wadogo binafsi wa umeme ili miradi hiyo ichangie katika kiasi cha umeme kinachozalishwa katika gridi ya taifa .

Mhandisi Mwijage ameweka wazi umuhimu wa wazalishaji wadogo wa umeme, katika maendeleo ya wananchi, na kusema serikali itaendelea kushirikiana nao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles