27.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 5, 2023

Contact us: [email protected]

RUTO AMUITA RAILA YOSHUA BANDIA

NAIROBI, KENYA

NAIBU Rais William Ruto amesema mgombea urais wa muungano wa upinzani wa NASA, Raila Odinga ni Yoshua bandia.

Akiwa ameambatana na Rais Uhuru Kenyatta, Gavana wa Bungoma, Ken Lusaka pamoja na Waziri wa Maji Eugen Wamalwa kwenye kampeni mjini Kitale, Ruto pia alisema Ilani ya Nasa imeandikwa na ‘matapeli’ wa rasilimali za taifa hili.

“Raila Odinga ni Yoshua bandia anayeelekeza Wakenya kwenye Kanaani bandia, ambayo haina maziwa na asali bali ina mito chang’aa,” alisema Ruto akikejeli wapinzani wao wakuu ambao ni Raila na Kalonzo Musyoka wa Wiper.

Odinga tangu arudi kutoka Israel amekuwa akijiita Yoshua wa Biblia, ambaye aliwaongoza Waisrael katika nchi mpya ya Kanaani yenye utajiri wa rasilimali.

Na amekuwa akiwaahidi Wakenya kuwa utawala wake utaruhusu pombe za kienyeji zilizoharamishwa kama vile chang’aa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles