26.7 C
Dar es Salaam
Thursday, September 21, 2023

Contact us: [email protected]

MATOKEO KIDATO CHA SITA YAWATISHA MADIWANI

Na FLORENCE SANAWA-TANDAHIMBA

MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba, Mkoa wa Mtwara, wamesikitishwa na matokeo ya kidato cha sita ya Shule ya Sekondari Tandahimba.

Masikitiko hayo yamekuja baada ya shule hiyo kutokuwa kwenye orodha ya shule kumi bora katika matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa hivi karibuni.

Akizungumza wakati wa kikao cha baraza la madiwani juzi, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mihambwe, Namkurya Seleman (CUF), alisema matokeo hayo hayajawaridhisha na kwamba zinatakiwa nguvu za ziada ili kupandisha kiwango cha elimu wilayani humo.

Alisema kitendo cha shule hiyo kushuka kutoka kumi bora wakati wa matokeo ya mwaka jana hadi nafasi ya 32 mwaka huu, kimekera na hivyo kulazimika kuunda kamati ya uchunguzi ili kujua tatizo la kushuka kwa kiwango cha ufaulu.

“Hii kamati niliyounda itasikiliza walimu moja kwa moja ili kujua matatizo yao ingawa inawezekana kitendo cha walimu kubadilishwa badilishwa kinaweza kuwa chanzo cha kushuka kwa matokeo hayo.

“Tutakapojua chanzo cha tatizo, tutaweza kujua jinsi ya kulitatua ili shule yetu iweze kuendelea kufanya vizuri kama ilivyofanya mwaka jana.

“Shule ya kidato cha tano na sita iko moja hapa wilayani na inapofanya vizuri, hata sisi pia tunajisikia vizuri ndio maana inaposhuka, madiwani wanahoji ni kwanini imekuwa hivyo,” alisema Namkurya.

 

Naye Ofisa Elimu Sekondari, Wilaya ya Tandahimba, Sostenes Luhende, alisema matokeo ya shule hiyo si mabaya kwa kuwa hakuna mwanafunzi aliyepata daraja la nne wala daraja sifuri.

Kwa mujibu wa Luhende, wanafunzi wamekuwa wakisoma katika mazingira magumu kwa kuwa hawana maeneo mazuri ya kujisomea ikiwamo maktaba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles