32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, February 5, 2023

Contact us: [email protected]

Rodgers akataa kuifundisha England

Brendan Rodgers
Brendan Rodgers

MANCHESTER, ENGLAND

KOCHA wa zamani wa klabu ya England, Brendan Rodgers, amekataa kuifundisha timu ya taifa ya England na amedai kwamba ndoto zake kwa sasa ni kuifundisha klabu ya Celtic ya nchini Scotland.

Kocha Roy Hodgson, ameamua kuachana na timu hiyo ya taifa ya England mara baada ya kutolewa katika michuano ya Kombe la Euro 2016 nchini Ufaransa, hivyo baadhi ya makocha ambao wametajwa kuchukua nafasi ya Hodgson ni Rodgers.

Hata hivyo, Rodgers tayari amesaini mkataba wa kuifundisha klabu ya Celtic na amesema hawezi kuachana na klabu hiyo kwa ajili ya England.

“Nilikuwa shabiki wa Celtic kwa muda mrefu na sasa nimekuwa kocha wa timu hii, ni ndoto kwangu ya muda mrefu lakini sasa imekamilika na ninafuraha kubwa kuwa kocha wa timu hii ambayo ina mashabiki wengi.

“England ni timu kubwa duniani na ina wachezaji wenye uwezo mkubwa na majina makubwa, lakini sina mpango wa kuwa kocha wa timu hiyo ninaamini ni timu ngumu kwa mimi kuifundisha.

“Nimeshangaa kuona kocha Hodgson kuachana na timu hiyo, ninaamini ana uwezo mkubwa sana, hivyo siwezi kufanya makubwa kama ambavyo yeye amefanya japokuwa kuna watu wanaamini naweza kufanya hivyo,” alisema Rodgers.

Hata hivyo, tayari timu hiyo ya England imefanikiwa kupata kocha wa muda, Gareth Southgate, ambaye atakuwa ndani ya timu hiyo hadi pale kocha mpya atakapopatikana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles