24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

RC Makonda afanyiwa dua maalumu Dar

makonda-559x520Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amefanyiwa dua maalumu ya kumuombea aweze kutimiza majukumu yake aliyokabidhiwa na Rais Dk. John Magufuli ya kuongoza mkoa huo.

Dua hiyo ilifanyika jana katika kituo cha maombi kinachosimamiwa na Sheikh Chifu Msopa maarufu kwa jina la Sharif Majini.

Sheikh Msopa lisema anaamini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mkuu huyo wa mkoa ataweza kuhimili majukumu yake aliyopewa akiwa katika umri wa ujana ikiwa ni pamoja na kutenda haki kwa wananchi wote.

Akizungumza kwenye ofisi za Kituo cha Maombi kilichopo Mabibo mwisho,   Dar es Salaam, Sheikh Msopa,  alisema lengo kuu la dua hiyo ni kuhakikisha Makonda anaendelea kutimiza wajibu  wake kwa kumtanguliza Mungu.

“Leo (jana), tumeamua kufanya dua nzito kwa ajili ya  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na dua hii ni  kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ampe afya njema, ampe  hekima na busara kwenye kutimiza majukumu yake.

“Hakuna asiyejua changamoto za Mkoa  huu wa Dar es Salaam ambao una watu wengi na mambo mengi lakini pia ndiyo kioo cha nchi.

“Kwa hali hiyo na kwa dhati kabisa tumeamua kuendesha dua hii ambayo wananchi mbalimbali wamedhudhuria kama manavyoona,” alisema Sheikh Msopa.

Alisema Makonda amekuwa ni mmoja wa viongozi vijana  wenye uwezo tangu alipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni  ambako amefanya kazi kubwa ikiwamo kuwa mbunifu kwa ajili ya wananchi  anaowaongoza.

Sheikh Msopa  alisema kwa hali hiyo viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya   kuendesha maombi kwa viongozi waliopewa nafasi  ili Mwenyezi Mungu awafanyie wepesi kwa kutimiza majukumu yao ya  utendaji na kwa haki.

“Makonda ni aina ya kiongozi ambaye siku zote anasimama kwenye haki na ndiyo maana ameweza kutatua migogoro mingi  iliyokuwa inatokea kwenye Wilaya ya Kinondoni na sasa amekabidhi ukuu wa mkoa tunaamini Mungu atamuongoza zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles